USIENDELEE KUKAA NA MAKOSA KWENYE JENGO AMBAYO HUKUDHAMIRIA.

Japo ni kweli kwamba kufanya marekebisho yoyote ya ujenzi yanahusisha gharama ambayo mara nyingine haipo hata kwenye bajeti. Lakini ni kulihujumu na kulipunguzia jengo hadhi pale unapoamua kupuuza makosa makubwa yaliyopo kwenye jengo. Ubora na hadhi ya jengo inaongeza mpaka hamasa na shauku ya watu wanaolitumia jengo hilo kiasi kwamba inaongeza hata ile “self-esteem” na mafanikio kwenye maisha kwa ujumla.

House improvement concept. Rear view of Asian construction worker looking away.

Jengo linapokuwa limekosewa linapoteza mpaka ule mtiririko wa kimatumizi ambao unaathiri ule utaratibu wa kawaida wa maisha ya kila siku ambao huwa unazingatiwa kanuni zake wakati jengo linabuniwa au kusanifiwa. Kwa hiyo jengo linapokuwa limekosewa, makosa yake huonekana moja kwa moja kupitia matumizi ya kila siku ya jengo kwa watumiaji. Makosa ambayo huathiri hata ufanisi wa kazi za watumiaji wa jengo kwa namna moja au nyingine.

Hivyo ni muhimu na sahihi sana kuhakikisha kwamba makosa yeyote yaliyofanyika kwenye jengo wakati wa ujenzi au wakati ubunifu wa jengo aidha kwa makusudi au kwa bahati mbaya yanarekebishwa. Hii ni kwa sababu makosa haya kwanza yanashusha hadhi ya jengo au kuathiri matumizi ya jengo hilo kwa watumiaji. Hii ni kwa sababu kuna gharama kubwa sana imetumika katika mchakato mzima wa ujenzi kwa ujumla, gharama ambayo imelengwa kuhakikisha jengo linajengwa kwa hadhi ambayo inaendana na hadhi ya watumiaji, hivyo ikiwa makosa hayo hayatarekebishwa itakuwa sio tu kutowatendea haki watumiaji bali jengo litapoteza hata baadhi ya watumiaji ambao aidha kwa kuona au kutokuona makosa hayo wataona sio la hadhi yao.

Karibu sana.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255 717 452 790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *