AINA TOFAUTI ZA MAJENGO KWENYE GHARAMA ZINATOFAUTIANA KWENYE UKAMILISHAJI(FIISHING).

Ukifuatilia viwango vilivyowekwa na bodi mbalimbali za gharama na hasa bodi za ujenzi utakuta kwamba gharama za ujenzi kwa mita moja za mraba zimewekwa kwa makundi mbalimbali ya gharama kwamba majengo yako na gharama tofauti kulingana na malengo yake na matumizi yaliyokusudiwa. Kwa mfano utakuja ujenzi wa nyumba ya kuishi gharama yake ni tofauti na ujenzi wa madarasa au shule, hali kadhalika ujenzi wa jengo la hoteli gharama yake ni tofauti na ujenzi wa jengo la kanisa au hata nyumba ya kuishi. Hata ujenzi wa ukumbi bado utakuta gharama ya kujenga mita moja za mraba ni tofauti na ujenzi wa jengo la karakana au godown.

Japo gharama hizi zinachangiwa na mambo mbalimbali ikiwemo wingi wa vyumba ndani ya jengo ambavyo vinaletwa na wingi wa kuta zilizotumika kugawanya vyumba hivyo lakini ukiachana na utofauti wa aina hiyo utofauti mkuu wa gharama hata kwa majengo yanayofanana unatokea kwenye hatua ya ukamilishaji(finishing). Ukamilishaji wa jengo au maarufu kama “finishing” ambao ni hatua inayofuata baada ya kumaliza kujenga mihimili yote ya jengo mpaka kupaua ni hatua inayoleta utofauti mkubwa wa gharama. Hii ni kwa sababu hatua ya mhimili hufanana kwa sehemu kubwa na vifaa vinavyotumika havina utofauti mkubwa sana lakini hatua ya umaliziaji huwa nan jia nyingi mbadala na vifaa vyenye viwango na hadhi tofauti tofauti.

Jambo la msingi la kujua hapa ni kwamba majengo yanatofautiana gharama kulingana na aina ya jengo na matumizi yaliyokusudiwa lakini sehemu kubwa ya utofauti huo upo kwenye hatua ya ujenzi ya umaliziaji kwani ndilo eneo ambalo lina njia nyingi mbadala za kuamua kuchukua ambazo utofauti wake uko zaidi kwenye gharama za vifaa na hata ufundi pia. Majengo ya shughuli za starehe zaidi kama vile mahoteli, kumbi za disco, kumbi za starehe na mikutano, mabaa na migahawa n.k., zina gharama kubwa zaidi kwenye umaliziaji ukilinganisha na majengo ya kazi kama vile karakana, viwanda, mashule, masoko n.k., Lakini pia umaridadi na ugumu wa ujenzi huongeza zaidi gharama kwenye ufundi hivyo kufanya baadhi ya aina hizo kuwa tena na gharama zaidi.

Karibu sana.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255 717 452 790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *