CHANGAMOTO ZA USIMAMIZI WA MRADI WA UJENZI.

Watu wengi kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kudhibiti na kujaribu kupunguza gharama huchagua kusimamia miradi yao ya ujenzi wenyewe. Hakuna ubaya wowote kwenye kusimamia mradi wako wa ujenzi mwenyewe na kimsingi itakusaidia sana katika kuuelewa vizuri ujenzi ambao wengi hawauelewi. Na zaidi ya hapo ni kwamba kama utakuwa makini vizuri na kutumia akili sana kusimamia mradi wako wa ujenzi mwenyewe kweli kutasaidia pia katika kupunguza gharama za ujenzi.

Lakini pia kabla ya kuamua kufanya hivyo inabidi kufahamu changamoto zake pia. Kitu cha kwanza na muhimu sana katika hili ni suala zima la muda, yaani kama utaamua kusimamia mradi wako wa ujenzi hakikisha una muda wa kutosha kufuatilia mambo mengi sana na kupatikana kwa wakati mra zote. Mradi wa ujenzi unahusisha sana ufuatiliaji mkubwa na wakati mwingine pia wa kina sana na kufahamu mambo mengi muhimu ambayo utapaswa kuyafanyia maamuzi sahihi ikiwa wewe ndio umeamua kuwa msimamizi mkuu. Hivyo unatakiwa uwe unapatikana muda mwingi wakati mradi unaendelea yaani uwe kama wewe ndiye mjenzi kuhakikisha kila kitu kinapatikana ndani ya muda na kwa usahihi kuepuka kuingia hasara.

Multi ethnic factory engineers checking digital tablet at factory warehouse

Jambo la pili ambalo nalo ni muhimu sana ni uelewa ili kuepuka kupotoshwa au kudanganywa. Ukiwa umeamua kusimamia mradi wako wa ujenzi mwenyewe unapaswa kuwa na uelewa wa mambo mengi sana kwani wale unaowatumia watajua kwamba huna uelewa wa mambo mengi hivyo wataona hiyo ni fursa yao kunufaika kupitia kukupotosha wewe ambaye kuna mambo ambayo wanajua sio rahisi uyafahamu lakini yenye maslahi kwao kwa gharama ya kukuumiza wewe. Hivyo kupunguza uwezekano huu wa kupotoshwa na kuibiwa unapaswa kuwa na watu wengi tofuati tofauti wa kuwauliza kitu kimoja ukijaribu kulinganisha majibu au maelezo yao kuweza kujua uhalisia kwa ajili ya kufanya maamuzi muhimu. Hata hivyo kama usipopata watu waaminifu basi ni vigumu sana kuepuka kupotoshwa na watu kunufaika na wewe.

Changamoto ya tatu kubwa ni kupotoshwa kwenye mambo ambayo ni ya kitaalamu ili watu kuweza kunufaika kwa aidha kufanya kazi kiurahisi au kutotumia watu wenye uwezo mkubwa katika eneo husika ili kukwepa au kupunguza gharama. Hili japo ni hatari huwa ndio rahisi zaidi kupotoshwa na watu kunufaika kwa sababu ni gumu hata kwenye ufuatiliaji kutokana na kwamba ukweli wake ni vigumu sana kujulikana kwani kesi mbalimbali zinatofautiana, hakuna ufanano.

Karibu sana.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255 717 452 790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *