MUDA NI FEDHA, KASI NI THAMANI.
Kadiri kitu kinavyoweza kufanyika kwa haraka zaidi lakini kwa ubora ule ule gharama ya kukikamilisha huwa inakuwa kubwa zaidi kuliko kinapofanyika kwa kutumia muda mrefu zaidi. Mfano mzuri ni kwenye usafiri, kwamba pamoja na mambo mengine kama vile usalama na mazingira bora ya ndani ya chombo cha usafiri, lakini usafiri unaowahi zaidi huwa na gharama kubwa zaidi ukilinganisha na usafiri unaochelewa na thamani ya ziada hapo ni muda unaookolewa.
Tukija kwenye ujenzi pia mambo hayako tofauti sana, pale ambapo ubora wa kazi na rasilimali ziko sawa mkandarasi anayeweza kukamilisha mradi kwa muda mchache zaidi kwanza ni yule mwenye uzoefu zaidi na uwezo zaidi, lakini pia ndiye anayechukuliwa ni wa thamani zaidi kwani anakuwa ameokoa rasilimali muda ambayo inaleta manufaa mengine kama vile jengo kuanza kutumika mapema zaidi na kufanikisha malengo yaliyokusudiwa kwa haraka zaidi.
Ikiwa unahitaji kufanya kazi yako kwa haraka zaidi lakini kwa ubora na kwa viwango vya juu lakini kwa gharama za kawaida zisizolazimu kuongezeka kwa sababu ya kasi ambayo ni thamani ya ziada unaweza kuwasiliana nasi tukakupatia watalaamu wenye ubobeza mkubwa katika kuokoa muda lakini huku wakizingatia viwango vya ubora wa hali ya juu.
Architect Sebastian Moshi
Whatsapp/Call +255717452790
Leave a Reply
Want to join the discussion?Feel free to contribute!