KIASI CHA MWINUKO KINACHOFAA KWA “BASEMENT” KWENYE UJENZI.

Miaka ya nyuma kidogo wakati taaluma ya ujenzi bado haijapiga hatua kubwa sana kwa kuwa na upungufu mkubwa wa wataalamu kuna mawazo mengi yalikuwa hayafanyiwi kazi au wakati mwingine hata kujulikana kabisa. Hili lilichangiwa pia na watu kutokuwa na uzoefu katika maeneo mengine ya dunia sambamba na teknolojia ya ujenzi kuwa duni sana ukilinganisha na sasa. Lakini kwa sasa kuna mambo mengi yanaendelea kufanyika na mambo mengine mengi zaidi na mazuri yanaendelea kugundulika katika kuimarisha sana tasnia hii ya ujenzi.

Mfano wa teknolojia ambayo haikuwepo ni pamoja na hii ya kutengeneza vyumba katika eneo chini la nyumba ambalo kwa zamani lilikuwa linafanywa msingi mkubwa ambao umejazwa sana na kugharimu gharama kubwa sana ili kupata ile tambarare ya eneo la sakafu ya chini. Lakini baada ya watu kugundua kwamba eneo hilo badala ya kutumia gharama kubwa kulijaza kama sehemu ya nyumba ni vyumba likageuzwa kuwa ni vyumba ikawa ni faida kwa upande huo.

Hivyo sasa baadaye ikawa watu wengi wanachukua njia hii na mpaka sasa nyumba nyingi kwenye maeneo ya mteremko na miinuko yamefanywa kama nusu ghorofa kwa kujengwa sakafu ya chini “basement floor”. Lakini pamoja na hayo bado sio kila mwinuko unaweza kupata nafasi hii ya kutengenezewa sakafu ya chini kwenye eneo ambalo badala yake lingekuwa ni msingi wa jengo. Eneo linahitaji kuwa na kina fulani cha urefu kuweza kufaa kwa njia hii tofauti na baadhi ya watu ambao hutaka sana kufanya hivyo katika eneo ambalo kina chake hakijafikia kufanya hivyo.

Hata hivyo kwa kupitia kulazimisha njia hiyo hata eneo ambalo kina chake hakijafikia bado inaweza kulazimishiwa njia hiyo lakini kwa kutumia gharama kubwa sana ya kutengeneza mazingira hayo. Ikiwa unahitaji kufahamu kama eneo lake limetimiza vigezo hivyo unapaswa kuchukua mtaalamu wa usanifu majengo na kufika naye eneo hilo la kiwanja chako mkajadili na kufikia maamuzi.

Karibu sana.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255 717 452 790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *