Entries by Ujenzi Makini

KUBOMOA NYUMBA NA KUYATUMIA TENA MABATI AU VIGAE VYA NYUMBA YAKO.

Mara nyingi watu wamekuwa aidha wakibomoa nyumba au wakiendeleza nyumba au kukarabati nyumba kwa namna ambayo inahusisha kuondoa kwanza bati za nyumba hiyo. Kuondoa huku bati au malighafi nyingine iliyotumika kutengeneza paa kama vile vigae kumekuwa kunadhaniwa na watu wengi kwamba inalazimu mtu aweke paa jingine jipya kabisa kwa kuwa lile linakuwa limeshaharibika. Kwa mfano […]

TABIRI MRADI WAKO WA UJENZI KWA KUTUMIA MFUMO.

Miradi ya ujenzi hasa miradi midogo na ya saizi ya kati imekuwa ni miradi isiyoisha changamoto katika mchakato wa ujenzi wake kwa sababu ya utata mwingi uliopo katika mfumo mzima wa uendeshaji. Utata wa miradi ya ujenzi inaanzia kuanzia kwenye uaminifu, uwezo, uzoefu na uzingatiaji wa taaluma husika za ujenzi katika vitengo husika. Mjumuisho wa […]

USALAMA PEKEE KWENYE UJENZI NI KUZINGATIA KUFANYA KAZI NA WATU WAAMINIFU.

Kadiri ninavyoendelea kufanya usimamizi wa miradi ya ujenzi na kujifunza zaidi na zaidi na kufanya uchunguzi wa kina ndivyo ninavyozidi kushawishika kwamba suala la kufanya kazi na watu waaminifu haliepukiki ikiwa kweli unahitaji kukamilisha mradi wenye thamani kubwa. Ni kweli kabisa na ni muhimu sana kudhibiti uharibifu na ubadhirifu wa namna mbalimbali katika eneo la […]

NAANDIKA KUTOKA KWENYE UZOEFU BINAFSI.

Baadhi ya watu wamekuwa wakihoji kuhusu makala zinazokwenda hewani hapa kwenye tovuti zinaandikwa kutoka kwenye chanzo gani cha taarifa. Ni kweli kwamba hizi makala bado zinaendelea kuja sana tena zinaongeza kasi ya ujio wake japo tunataka kuziboresha zaidi ili ziwe zinagusa sana watu kwa namna zote hizi tofauti. Hata hivyo makala hizi zinaandikwa kutoka kwenye […]

BAADHI YA WATU WENGI WALIOJENGA KWA RAMANI ZA KWENYE MITANDAO BILA KUHUSISHA MTAALAMU WAMEISHIA KWENYE MAJUTO.

Kuna watu wanaamini kwamba ramani za kujenga nyumba zinapatikana kwenye mitandao, wakati mwingine ni ushauri kutoka kwa marafiki au watu wa karibu kwamba kama unataka kujenga nyumba unaweza kuchukua ramani kwenye mitandao. Ukweli ni kwamba kuna uwezekano wa zaidi ya asilimia 95% kwamba ramani unayoitoa kwenye mitadao haikufai, hata kama umeinunua kwa pesa kama aliyekuuzia […]