Entries by Ujenzi Makini

KABLA YA KUPAUA JENGO.

Changamoto kubwa sana tunazokutana nazo kwenye ujenzi huwa zinatuathiri kwa sababu mara nyingi huwa hatuzitegemei kutokea bali zinakuja kwa kama ajali katika wakati ambao pengine tumeshachelewa au tunahitaji kutatua kwa gharama kubwa sana. Na moja kati ya sababu ya changamoto hizo kujitokeza ukiachilia mbali uzembe na ubadhirifu basi huwa ni kukosa ushirikiano kama timu ya […]

UJENZI UNAPOKOSA WATAALAMU NA THAMANI INAKOSEKANA PIA.

Siku za hivi karibuni nilifanya kikao na ofisa mmoja wa mikopo wa moja kati ya benki za kigeni zinafanya vizuri sana hapa nchini. Tuliweza kuongea mengi na mimi nikijaribu kumpa maelezo ya mapendekezo yangu kwake ndio tukajikuta tumeingia kwenye mjadala mmoja uoavutia sana. Aliniambia kwamba wamekuwa wakitoa mikopo ya ujenzi kwa mashirika na kwa watu […]

IKIWA UNAPATA CHANGAMOTO ZA KUPATA WATU WAAMINIFU WA KUFANYA NAO KAZI KARIBU.

Kama nilivyotangulia kusema kwenye makala zilizopita linapokuja suala la ujenzi basi tabia ya uaminifu kwa fundi au mkandarasi anayepewa kazi ni jambo la lazima ikiwa unahitaji mradi wa ujenzi umalizike vizuri na kwa amani bila mivutano na ubabaishaji. Lakini changamoto ni kwamba tabia ya uaminifu ndio tabia adimu zaidi katika tabia za watu, inachukua muda […]

KIBALI CHA UJENZI KINACHUKUA MUDA GANI KWA MCHAKATO MZIMA KUKAMILIKA?

Mamlaka mbalimbali za serikali pamoja na nyingine zisizo na uhusiano wa moja kwa moja na serikali zimeendelea kuboreshwa na kutanuka zaidi katika kuwapelekea watu huduma karibu sana na wao ili pia kuweza kudhibiti mambo yafanyike kwa kufuata utaratibu uliowekwa. Kutokana na kutanuka sana kwa mamlaka hizi basi watu wengi sana siku wanajitahidi kujiongeza kwa kufuatilia […]

ANZA MRADI WAKO WA UJENZI UTAMALIZA.

Kutoka kwenye uzoefu wa watu wengi sana niliokutana nao mara nyingi watu huanza miradi yao ya ujenzi wakiwa hawana uhakika kama wanakwenda kukamilisha miradi hiyo na huanza kama utani tu wakiwa hawajui ni lini watakamilisha miradi yao. Lakini kwa sababu baada ya mtu kuanza huweka nguvu na akili zake zote kwenye mradi huo wa ujenzi […]