Entries by Ujenzi Makini

MLIMA KAMA KAZI KATI YA MTAALAMU ALIYEFANYA MICHORO YA RAMANI NA FUNDI AU MKANDARASI.

Imekuwa kawaida kwa watu kutafuta namna ya kukamilisha hatua ya kutengeneza michoro ya ramani kwa ajili ya ujenzi wa mradi wake wa ujenzi wakati mwingine wengine wanadiriki hata kuiba au kuchukua mitandaoni bila kujali madhara makubwa na hasara inayoambatana na kupata ramani bila kuhusika kwa mtaalamu wa usanifu. Kwa watu wengi wakishakamilisha kupata michoro ya […]

GHARAMA YA UJENZI ULIOPEWA NI MAKADIRIO TU.

Unaweza kufurahia au kuumizwa na gharama ya ujenzi uliopewa kwa kuiangalia kwa sababu umeamini kwamba hiyo ndio gharama inayokwenda kumaliza kazi yako. Nachopenda kukushauri ni kwamba hutakiwi kufurahia wala kuumizwa na gharama ya ujenzi unayopewa na fundi au mkandarasi kwa ajili ya kukujengea jengo lako kwa sababu kwa sehemu kubwa hiyo sio gharama halisi. Na […]

UJENZI NI UTAALAMU NA UZOEFU.

Moja kati ya changamoto ambayo huwakuta wataalamu waliomaliza chuo siku za karibuni na kuingia kwenye kazi za ujenzi ni pamoja na kuwa na uwezo mdogo kwenye kazi za ufundi wa ujenzi. Suala la wataalamu wa ujenzi kuwa na uwezo mdogo katika shughuli za ujenzi haliwaathiri vijana waliotoka chuoni peke yake bali hata wataalamu wakongwe ambao […]

MCHAKATO WA KUPATA KIBALI CHA UJENZI.

Juzi nimepigiwa simu na binamu yangu mmoja ambaye alikuwa anajulisha kwamba anataka uchukua kibali cha ujenzi ili aweze kuanza kujenzi wa nyumba yake katika eneo analoishi bila kukutana na bugdha wala usumbufu wa aina yoyote kutoka kwenye mamlaka husika. Binamu yangu alinipigia akaniamba, “Seba nataka nichukue kibali cha ujenzi, hivi nahitajika nini na nini”, mimi […]

HATUA YA KWANZA MUHIMU KWENYE UJENZI

Mara kwa mara nimekuwa ninaeleza hapa umuhimu wa kuwepo kwa mtaalamu kwenye usimamizi wa ujenzi kuhakikisha kwamba utaalamu unazingatiwa na kile kilichokusudiwa kinapatikana kwa uhakika. Kweli haya yanawezekana ikiwa kuna aidha mpango au mchakato unaofuatwa katika kufanyia kazi mradi husika au kuna mtaalamu ambaye anafahamu na anafanya maamuzi sahihi kwenye kila hatua ya ujenzi mara […]

UJENZI WA TOFALI ZA KUCHOMA DAR ES SALAAM.

Tofali za kuchoma zimekuwa zikitumika zaidi na kukubalika maeneo mbalimbali duniani. Hata hivyo kwa Tanzania zimekuwa zikitumika zaidi yale maeneo au mikoa ambapo zinapatikana kwa urahisi. Lakini watu mbalimbali, kwa sababu mbalimbali wamekuwa wakizipenda na kutamani kuzitumia sio tu kwenye maeneo zinakopaatikana kwa urahisi bali hata kwenye mikoa na miji ambapo hazipatikani kiurahisi. Jambo hili […]

MRADI WA UJENZI UWEKEWE VIWANGO KABLA YA KAZI KUANZA.

Licha ya kwamba siku hizi kumekuwa na na maendeleo makubwa ya kiteknolojia na kitaaluma ambayo yamepelekea kufanyika kwa kazi za michoro zinazoonyesha kila kitu kinachokwenda kufanyika kitakavyokuwa kabla hata ya ujenzi kuanza lakini bado kumekuwa na changamoto ya wahusika kufikia viwango ambavyo vinatarajiwa kwenye kazi za ujenzi. Jambo hili limekuwa likichangiwa na kutokuwepo kwa makubalianao […]