Entries by Ujenzi Makini

KUONGEZA THAMANI YA JENGO KATIKA HATUA YA UJENZI.

Changamoto kubwa katika fani ya ujenzi katika eneo la ubora na thamani ipo zaidi kwenye miradi midogo midogo kwa sababu ndio eneo ambalo miradi hii haifuati taratibu mbalimbali za kitaalamu zilizowekwa kwa sababu mbalimbali. Sababu kuu ya watu wengi ni gharama lakini sababu nyingine ya ndani zaidi ni kukosekana kwa uelewa wa hatari na madhara […]

USIOGOPE KUANZA UJENZI, ANZA NA RAMANI.

Kuna watu wengi sana hasa vijana hutamani sana kujenga lakini wanapoulizia gharama za ujenzi na kuambiwa hukata tamaa na kuamua kuahirisha kabisa kujenga. Ukweli ni kwamba gharama za ujenzi ni kubwa ukilinganisha na kipato cha watu walio wengi wa kipato cha kati. Hivyo mtu anapoangalia kipato chake kwa mwezi akilinganisha na gharama za ujenzi hukata […]

UNAWEZA KUFANYIWA RAMANI NYINGINE YA UJENZI NZURI ZAIDI YA HIYO.

Watu wengi wamekuwa wanapata changamoto kwenye kuelewa kitu kimoja katika ujenzi kwamba picha au ramani uliyoiona haikutengenezwa kwa ajili yako na hivyo sio rahisi ikufae na kwamba utaweza kupata manufaa mengi utakapofanyiwa kazi mpya inayoendana na mawazo tuliyonayo. Kuna watu pia hufikiri kwamba ramani nyumba wanayoiona inaweza kufanyiwa kazi ikibaki hivyo hivyo na ikajengwa bila […]

MAAMUZI SAHIHI KWENYE UJENZI YANAHITAJI UKOMAVU WA KIAKILI TUNAOUITA BUSARA.

Katika zama za zamani za Misri, Ugiriki na Roma kulikuwa hakuna utofauti unaoelezeka kwa usahihi kati ya maneno busara na usomi. Mara nyingi usomi uliitwa au kufananishwa neno busara kama linavyofahamika katika nyakati za sasa. Pengine hili lilitokana na kwamba watu wengi waliojihangaisha kusoma katika nyakati za zamani walikuwa ni wale waliokuwa na busara kubwa […]