Entries by Ujenzi Makini

KUHUSU UJENZI HUPASWI KUKATA TAMAA.

Watu wengi wanapokuwa vijana wadogo wanaokua huwa na ndoto kubwa sana kwenye maisha yao za kufanikisha mambo mengi sana makubwa. Lakini kwa bahati mbaya wengi ndoto zao huendelea kufifia kadiri ziko zinavyoendelea Kwenda mbele, japo baadhi hujitahidi kupambana nazo kwa nguvu lakini bado kuna kundi kubwa ambalo huishia kukata tamaa kadiri miaka inavyozidi kwenda mbele. […]

GHARAMA ZA UJENZI WA NYUMBA.

Wote tunafahamu kwamba ujenzi wa nyumba ni jambo linalohusisha gharama kubwa, na kwa watu wengi ndio mradi wa gharama kubwa kuliko kitu kingine chochote katika maisha. Sababu hii imepelekea kwamba watu wengi kuogopa sana gharama za ujenzi kiasi kwamba mara zote wamekuwa wakifikiri namna ya kupata ujenzi wa bei nafuu. Hata hivyo kwa kupitia njia […]

UJENZI WA GHOROFA KWA BEI NAFUU.

Wako watu wengi sana kwa sasa wanaotamani sana kujenga nyumba za ghorofa kwani wanaamini nyumba za ghorofa zinapendeza na kuvutia zaidi na zinasaidia katika kuokoa eneo la kiwanja ambalo lingejazwa kwa sehemu kubwa zaidi ikiwa mtu ataweka vyumba vyote katika sakafu moja. Lakini watu hawa wengi wamekuwa wakihofia kujenga nyumba ya ghorofa ya kuishi kwa […]

HII NI CHANGAMOTO KATIKA UJENZI.

Moja kati ya tamaduni ambazo tumekuzwa nazo lakini zinatugharimu sana hapa nchini ni pamoja na suala zima la ukweli na uwazi. Kwa miaka ya nyuma kwenye taasisi nyingi hususan za umma suala la uwazi wa taarifa na takwimu nyingine ndani ya taasisi hizo sio jambo lililokuwa linapewa kipaumbele. Inawezekana ni sababu za kisiasa au nyinginezo […]

RAMANI YA NYUMBA YAKO.

Imekuwa kawaida sasa kwa baadhi ya watu kutokana na kutokujua undani wa kazi za ramani za ujenzi wamekuwa wakipenda kazi fulani na kutaka kujua kama kazi hiyo inaweza kufanyika kama ilivyo, na ajabu zaidi ni kutaka ifanyike kama ilivyo. Kiuhalisia hakuna kazi rahisi katika design kama ambayo imeshapendekezwa, ninaposema rahisi simaanishi kwamba ni kazi ndogo […]

VIBALI VYA KUJENGA JENGO LA GHOROFA NA GHARAMA ZAKE.

Jengo la ghorofa linahitaji vibali vya ujenzi vya aina nyingi, kwanza linahitaji kibali cha ujenzi kutoka halmashauri. Kibali hiki kinachotokea kwenye halmashauri ya jiji, manispaa au mji husika ndio kibali chenye mambo mengi na ndicho huweza kupata vizuizi na kuchukua muda pia. Hata hivyo hiki ndio huwa kibali cha kwanza kupatikana kabla ya vyote. Kibali […]

UTAJISIKIAJE KAMA UTAJENGA NYUMBA AMBAYO NI MFANO WA KUIGWA?

Mtazamo wa mtu ni kitu chenye nguvu sana, hicho ndicho huathiri taswira yake nzima kwenye maisha, mtazamo ndio ambao hupelekea namna maisha ya mtu yanavyokuwa katika uhalisia. Hili suala la mtazamo limebadilisha maisha ya watu wengi kuelekea kule ambako wamekuwa wakifikiri zaidi na kuwa kile ambacho kimekuwa kikitawala mitazamo yao. Wanafalsafa wote duniani na dini […]