Entries by Ujenzi Makini

KARIBU UULIZE CHOCHOTE KUHUSIANA NA MASUALA YA UJENZI.

Kama jinsi ilivyo tovuti yetu ni kuelemisha na kutoa ufanunuzi wa mambo mbalimbali katika tasnia ya ujenzi kwa ujumla kuanzia mambo ambayo ni ya kitaalamu, ya kiufundi au hata taratibu nyingine zozote ndani ya taaluma ya ujenzi pamoja na mamlaka mbalimbali zinazohusika kusimamia sekta hii, tunakukaribisha uulize chochote au ufanunuzi juu ya jambo lolote ambalo […]

DHANA YA UNAFUU WA GHARAMA KWENYE UJENZI.

Linapokuja suala la ujenzi nimekuwa nikiwashauri watu mbalimbali wanapoamua kujenga waanze kuweka mkazo kwanza kwenye kile wanachokitaka na wale wanayopendelea katika nyumba zao badala ya kuweka mkazo kwenye gharama za ujenzi. Ni kweli nafahamu kwamba gharama ndio mwamuzi mkuu lakini naamini kwamba kwa mtu yeyote kuna vipaumbele vyake ambavyo ni muhimu sana ambavyo havipaswi kuwekewa […]

KUIGA RAMANI YA MTANDAONI NI KAZI NGUMU ZAIDI KULIKO KUFANYA MWENYEWE.

Kuna baadhi ya watu wamekuwa hawaelewi utaratibu wa kazi tunazofanya wala undani wake na kimakosa wamekuwa wanafikiri kazi tunazofanya hususan picha wanazoziona kwamba tunazitoa mitandaoni na kisha kuziendeleza au kuzitumia kama zilivyo. Mtazamo wa aina hii umekuwa ukituweka katika mazingira magumu kwa sababu umepelekea baadhi ya watu kufikiri kwamba kazi tunayofanya ni rahisi sana kwa […]

MSINGI WA JENGO UNAPOKOSEWA.

Kwa kawaida siku zote ujenzi huwa unaanza na kitu kinachoitwa “setting out”, yaani kuli-set jengo katika eneo sahihi ambapo litakaa. Hatua hii huwa ni muhimu sana kwani ndio inayoamua uelekeo wa jengo na namna linahusiana na kiwanja linapojengwa lakini muhimu zaidi ni hatua hii inapaswa kufanyika kwa umakini mkubwa ili kupata usahihi wa mraba wa […]

UKUBWA WA VYUMBA UNAVYOHITAJI.

Mara nyingi sana wateja wengi tunaokutana nao huwa hawana mawazo ya ni ukubwa gani wa vyumba na maeneo mengine ndani ya nyumba zao wanaouhitaji. Hii huwa inakuwa changamoto kidogo kwa mtaalamu kwa sababu ni vigumu kubashiri ukubwa ambao mteja anauhitaji kwa sababu inakuwa vigumu kujua uzoefu wake wa eneo analoishi na namna anachukulia ukubwa aliouzoea. […]

KWENYE MRADI WA UJENZI USIWEKE MTAZAMAJI MKOSOAJI WEKA MSIMAMIZI.

Moja kati ya maeneo ambayo yamekuwa yakifanyika makosa makubwa kwenye usimamizi wa miradi ya ujenzi ni namna ambayo msimamizi anahusiana na mtekelezaji au wajenzi katika mradi. Wateja wengi wamekuwa wakifanya maamuzi ya kuweka kuingia mkataba na fundi au mkandarasi kisha kuweka msimamizi ambaye atakuwa anahakikisha kazi inafanyika kwa usahihi na kwa viwango vinavyokubalika kwa kuzingatia […]