Entries by Ujenzi Makini

IKIWA UNATHAMINI UBORA KWENYE UJENZI, WEKEZA KWENYE USHAURI WA KITAALAMU.

Katika kufanya jambo lolote ni muhimu kufahamu sehemu ambayo inaleta matokeo muhimu zaidi ambayo unahitaji kuweka nguvu kubwa zaidi au umakini wa hali ya juu zaidi. Watu wengi wanapofikiria kuhusu ujenzi, japo kiuhalisia mwisho wa siku huwa wanahitaji sana ubora lakini huwa wakati wanafikiria kuhusu ujenzi hawafikirii sehemu sahihi ya kuweka nguvu na umakini zaidi […]

HUDUMA ZA UJENZI ZA BURE HAZINA THAMANI.

Ni kanuni ya asili kwamba vitu vinavyoweza kupatikana bure au hata kupatikana kwa urahisi sana basi thamni yake ni ndogo sana na wakati mwingine havina thamani kabisa. Hii ni kanuni ya asili ambayo sio tu kwamba nimejifunza kwenye nadharia ya vitabu bali imenitokea mara kadhaa kwenye kazi zangu za kila siku na hasa katika shughuli […]

BAJETI YA UJENZI ULIYOPANGA HAITATOSHA

Kati ya vitu ambavyo sisi binadamu tumekuwa tunapenda ni kitu kinaitwa uhakika kinachoambatana na usahihi wa vitu. Hata mawazo yetu watu wengi tukifikiria huwa tunafikiria katika uhakika na usahihi lakini kwa bahati mbaya dunia sivyo ilivyo, vitu vingi duniani huwa havina usahihi wala uhakika na ni mara chache sana kukuta kitu chochote kile chenye usahihi […]

USIPOTEZE MUDA KUFIKIRIA KAZI YOTE, UJENZI NI SAFARI NDEFU NA INA VITU VINGI.

Watu wengi wamekuwa wanasita sana kwenye kuchukua hatua yoyote kwa kufikiria sana jinsi ya kumaliza mradi mzima wa ujenzi tangu mwanzoni, kitu kinachopelekea watu kusita kuchukua hatua na wengine kuahirisha hata kujenga kwa wakati huo akisubiri siku ambayo atakuwa tayari amefanikisha mambo mengi sana kuhusu mradi huo na miaka mingi kupita kabla hajafanya hivyo. Kuna […]

HIFADHI VIZURI MICHORO YA RAMANI ZAKO ZA UJENZI UTAKUJA KUIHITAJI BAADAYE.

Moja kati ya nyaraka muhimu ambazo unapaswa kuzihifadhi vizuri kwa sababu utakuja kuzihitaji baadaye ni pamoja na michoro ya ramani. Hii ni kwa sababu usipohifadhi vizuri michoro ya ramani ikapotea au kuharibika sana utakuja kuhitaji kutengeneza upya michoro ya ramani ya nyumba yako, kazi ambayo ni ngumu zaidi kuliko hata kutengeneza michoro mipya na ambayo […]