Entries by Ujenzi Makini

KAZI YA UJENZI KATIKA HATUA YA “FINISHING”.

Japo ubora wa kazi ya ujenzi huhitaji umakini mkubwa tangu mwanzoni kabisa wa kazi husika na pia kazi ambayo haikujengwa kwa usahihi tangu mwanzoni madhara yake huendelea kuonekana mpaka mwishoni mwa kazi lakini hatua ya “finishing” huhitaji umakini mkubwa wa ziada kwa sababu ndio hubeba taswira ya mwisho ya nyumba. Licha ya kwamba gharama ya […]

KINACHOLIPIWA KWENYE HUDUMA ZA USHAURI WA KITAALAMU NA UJENZI NI MUDA NA THAMANI.

Kati ya vitu ambavyo vimekuwa vikishangaza sana duniani katika Ulimwengu wa biashara ya soko huria ni jinsi vitu vinaweza kutofautiana bei licha ya kufanana kabisa matumizi. Lakini licha ya baadhi ya watu kufikiri kuna tatizo lakini wale ambao wanaelewa namna asili inavyofanya kazi yake hawashangazwi na hilo kwa sababu asili siku zote huwa ina nguvu […]

SAIKOLOJIA YA MALIPO NA UBORA WA KAZI KWENYE UJENZI.

Sisi binadamu ni viumbe wa kisaikolojia ambapo saikolojia ni ile tabia na mienendo ya binadamu inayosukumwa na hisia mbalimbali zilizopo ndani ya mwili katika kuendea au kufanya jambo fulani kwa kulipa uzito fulani ambao ndio unaoamua kiasi na viwango vya ufanyaji wake. Imekuwa kawaida kwa baadhi ya watu kutaka kazi fulani ya usanifu na wakati […]

VIWANJA VINGI NI VYA MAKAZI PEKEE

Kupata kibali cha ujenzi limekuwa ni suala lenye changamoto kubwa kwa miradi mingi isiyo ya makazi kwa sababu viwanja vingi ni kwa matumizi ya makazi pekee. Hata hivyo katika kununua viwanja watu wengi japo huwa na mawazo ya kuendeleza maeneo husika kwa miradi ya aina tofauti lakini huwa hawajihangaishi sana kuchunguza matumizi ya eneo hilo. […]

USIMAMIZI SAHIHI WA MRADI WA UJENZI UTAKUEPUSHA NA USUMBUFU, MATESO NA MSONGO WA MAWAZO.

Moja kati ya gharama kubwa ambazo watu huingia bila kujua ni usumbufu na msongo wa mawazo ambao hupitia pale wanapoweka usimamizi usio sahihi kwenye mradi wa ujenzi na mambo mengi kufanyika chini ya kiwango au kusababisha hasara. Usimamizi sahihi licha ya kukupatia matokeo mazuri sana mwishoni lakini pia hukuepusha kuingia kwenye msongo wa mawazo na […]

CHANGAMOTO YA UMBALI KWENYE MIRADI YA UJENZI

Kwa miradi midogo ya ujenzi mara nyingi baadhi ya watu hoona kwamba pengine wanahitaji mtaalamu anayepatikana katika eneo au mji husika, ambapo mara nyingi ni kwa sababu ya kuhofia kwamba mtu anayetoka mbali atakuwa aidha na gharama kubwa au upatikanaji wake ni wa shida. Ni kweli kwamba mtu anayepatikana karibu anaweza kupatikana kiurahisi kwa sababu […]

KAZI YA UJENZI IPANGIWE MUDA WA KUFANYIKA KWA HARAKA KADIRI INAVYOWEZEKANA

Katika mchakato wa kupitia maombi ya zabuni za wakandarasi mbalimbali wa miradi ya ujenzi kuna vigezo kadhaa ambavyo hutumika katika kuchagua mkandarasi aliyeshinda zabuni na anayestahili kupewa kazi ya kujenga mradi husika. Moja kati ya vigezo muhimu ambavyo huangaliwa ili kutoa zabuni husika ni pamoja na muda ambao mkandarasi huyo ameutaja kwamba atakuwa amemaliza kazi […]