Entries by Ujenzi Makini

WEKA MPANGILIO SAHIHI WA KIMATUMIZI KATIKA KIWANJA CHAKO KADIRI YA UTAMADUNI WAKO NA MAHITAJI YAKO.

Mpangilio wa kimatumizi ni eneo muhimu sana la kulifanyia kazi kwa ukaribu, umakini na uangalifu pale unapokuwa unatengeneza michoro ya ramani kwa ajili ya nyumba yako ya kuishi. Mara nyingi watu wamekuwa wakimwachia mtaalamu wa usanifu kuamua namna atapangilia mwenyewe kadiri anavyofikiri inafaa kitaalamu bila kujua kwamba anayeenda kutumia eneo hilo sio mtaalamu bali ni […]

MUDA WA ZEGE KUMWAGILIWA MAJI(CURING) KATIKA JENGO NI ANGALAU SIKU 21.

Katika ujenzi hususan wa majengo, mifumo yote inayohusika na mihimili ya jengo hutumia zege ikiwa jengo husika halijatumia mihimili ya chuma. Hata hivyo majengo yanayojengwa kwa chuma ni machache sana ukilinganisha na majengo yanayojengwa kwa zege. Hivyo majengo mengi katika mifumo yake ya mihimili yaani nguzo(columns), maboriti(beams), zege ya sakafu(slabs) na ngazi hujengwa kwa kutumia […]

TOVUTI YETU YA UJENZI MAKINI NI KWA AJILI YA KUJIFUNZA KWA MAELEZO NA PICHA.

Katika tovuti yetu ya ujenzi makini tumekuwa tukiandika makala nyingi za aina mbalimbali kuanzia makala za kitaalamu, kiufundi, miongozo, maelekezo, ushauri n.k. Lakini pia tumekuwa tukiambatanisha na uhalisia katika picha ya vitu mbalimbali japo sio picha zote huendana na ujumbe moja kwa moja lakini angalau picha hizi huweza kujenga hamasa na kumjengea msomaji picha ya […]

KILA MAAMUZI UNAYOFANYA KATIKA UJENZI YANA FAIDA KUBWA MBELENI NA KINYUME CHAKE NI HASARA NA MAJUTO.

Nimekuwa nikisisitiza sana suala la kuzingatia ubora wa huduma katika kila hatua ya ujenzi. Hii ni kwa sababu nafahamu kwamba hakuna mtu aliyewahi kujutia huduma bora bila kujali alizipata kwa namna gani, kwa sababu huduma bora siku zote zitakupa furaha na ufahari baadaye. Hisia zinazotuingia na kututia hofu tukaogopa huduma bora kwa kuhofia kwa gharama […]