Entries by Ujenzi Makini

GHARAMA ZA “FINISHING” YA NYUMBA

Tulishajadili huko nyuma namna rahisi na haraka ya kuweza kujua wastani wa gharama za ujenzi wa jengo lolote kwa ujumla, kwamba unachukua gharama ya kuja mita moja ya mraba ya jengo husika kisha unaizidisha na idadi ya mita za mraba za jengo unalotaka kujenga na hapo utapata jumla yake ambayo ndio itakuwa wastani wa gharama […]

GHARAMA ZA VIBALI VYA UJENZI ZINABADILIKA

Kama tulivyozungumza awali vibali vya ujenzi vimegawanyika katika makundi mawili makubwa kwa mtu ambaye hayuko kwenye sekta ya ujenzi. Kuna vibali vinavyotolewa na halmashauri za jiji, manispaa au miji ambazo ndio huitwa vibali vya ujenzi na kuna vile vinavyotolewa na bodi za ujenzi kwa mfumo wa stika za ujenzi. Kibali cha ujenzi kutoka halmashauri ya […]

KUPATA KIBALI CHA UJENZI KWENYE ENEO LISILOPIMWA

Mambo mengi yanaendelea kubadilika kwa kasi katika sekta ya ujenzi kupitia mamlaka za udhibiti ambazo zinaendelea kuongeza masharti mbalimbali katika kufanikisha malengo yao mbalimbali ikiwa ni pamoja na kukusanya mapato zaidi. Zamani ilikuwa kujenga kwenye eneo ambalo bado halijapimwa haikuhitaji kupata kibali cha ujenzi kutoka halmashauri husika hata kama ni eneo lililopo kwenye mji mkubwa […]

GHARAMA ZA RAMANI YA GHOROFA ZIKO MARA MBILI

Nyumba nyingi zaidi zilizokuwa zinajengwa siku za nyuma ni nyumba za kawaida za kuishi zisizo za ghorofa kwa sababu aidha ya kipato au mazoea. Lakini miaka ya hivi karibuni nyumba za ghorofa zinazojengwa nazo zimekuwa nyingi sana na watu wengi sana siku hizi wanafikia maamuzi ya kuamua kujenga ghorofa kwa sababu mbalimbali. Ni kweli nyumba […]

USIKUBALI KAZI YA UJENZI ILIYOFANYWA CHINI YA KIWANGO.

Kazi yoyote ya ujenzi ambayo haina usimamizi unaofuata taratibu sahihi ubora wake unabaki kutegemea busara, nidhani na uwezo wa fundi husika. Changamoto kubwa ni kwamba watu wengi wanaweza kufanya kazi yenye ubora pale tu wanapolazimika kufanya hivyo mara nyingi wanapokuwa chini ya usimamizi madhubuti. Watu hawa wana uwezo wa kufanya kazi kwa viwango vya juu […]

ONGEZEKO LA GHARAMA NDOGO NDOGO WAKATI WA UJENZI(VARIATIONS) NI MUHIMU.

Katika miradi ya ujenzi kuna kitu kitaalamu tunaita(variations), ambalo ni ongezeko la gharama ndogo ndogo za ujenzi wakati mradi ukiwa unaendelea. Ongezeko hili la gharama ndogo ndogo za ujenzi hutokana na sababu mbalimbali kwa mfano maamuzi mapya yaliyopelekea mabadiliko kiasi ambayo yanaathiri bajeti iliyokuwa imepangwa, mabadiliko ya hali ya hewa hususan mvua kubwa ambayo hayakutarajiwa […]

RANGI ZA NYUMBA, NAMNA UNAWEZA KUZITUMIA KUENDANA NA MAANA ZAKE AU ISHARA ZAKE.

Watu wengi kwenye eneo la rangi hubaki njia panda, wakati wengine wanatamani kujua mpangilio sahihi wa rangi ili kuleta muonekano unaovutia wengine hutamani kujua maana za rangi ili kupangilia kufuatana na maana zake. Kimsingi rangi zimegawanyika katika makundi makuu mawili ambayo ni rangi zinawaka sana kama vile nyekundu, njano na rangi ya chungwa na rangi […]