Entries by Ujenzi Makini

KWA MRADI WA UJENZI UNAOENDESHWA BILA KUFUATA UTARATIBU ULIOWEKWA NA MAMLAKA HUSIKA KISHERIA INAPASWA AWEPO MTU WA KUFANYA MAAMUZI YA MWISHO.

Wote tunajua kwamba mamlaka za ujenzi zimeweka utaratibu unaotakiwa kufuatwa katika miradi ya ujenzi mpaka kufikia mtu mwenye maamuzi ya mwisho kabisa katika ujenzi pale inapokuwa inatakiwa. Kwa kawaida maamuzi mengi ya ujenzi na hasa ya kitaalamu hufanywa na mshauri wa kitaalamu wa eneo husika(consultancy) na kama hayupo basi atafanya msaidizi wake au mtu mwingine […]

ATHARI ZA KIMAZINGIRA ZA MRADI WA UJENZI.

Mradi wowote wa ujenzi huja na athari zake kimazingira kulingana na aina ya mradi husika. Athari zinatofautiana viwangoa mabpo kuna miradi mingine huja na athari hasi kidogo sana na mingine huja na athari hasi nyingi zaidi na kadiri mradi unapokuwa na athari nyingi sana hasi ndivyo kadiri unavyozidi kupoteza uhalali wa kuwa katika eneo husika […]

WATU WANAOHUSIKA KUFANYA MAAMUZI KWENYE MRADI WA UJENZI

Kutokana na kutokufahamu taratibu na madhara yanayoweza kusababishwa na ufanyaji wa maamuzi kiholela kwenye mradi wa ujenzi, imekuwa jambo la kawaida kwa watu kujifanyia maamuzi kwenye mradi wa ujenzi vile watakavyo. Hili limekuwa linakuja na gharama kubwa kwa sababu watu hawa wamekuwa wakifanya maamuzi wakiwa hawana taarifa za kutosha wala uzoefu na utaalamu wa jambo […]

KUJENGA KWA HATUA NI BORA KULIKO KUCHAKACHUA GHARAMA.

Watu wengi wanapofikia hatua ya kuamua kuanza ujenzi wakiwa tayari wameweka kiasi cha fedha ambacho walitegemea kingefanikisha kukamilisha mradi mzima wa ujenzi mara nyingi wanakuta fedha hiyo haitoshi na wanahitajika fedha zaidi pengine nyingi sana ukilinganisha na iliyopo. Sasa inapotokea watu wanapojikuta katika hali hii baadhi huamua kufikiria namna ya kupunguza gharama za ujenzi ziendana […]

MAENEO 9 YA USIMAMIZI KATIKA USIMAMIZI WA JUMLA WA MRADI WA UJENZI(PROJECT MANAGEMENT)

Wote tunakubaliana kwamba shughuli yoyote ya ujenzi inaweza kufanyika kwa viwango vya juu vya ubora au kwa viwango vya chini vya ubora kutegemeana na uwezo wa kiusimamizi(project management). Sasa usimamizi sahihi na kamili wa ujenzi unahusisha maeneo haya tisa. Usimamizi wa kuunganisha shughuli zote za ujenzi ziende katika utaratibu sahihi uliopangwa kwa ajili ya kufanikisha […]

USIMAMIZI WA MRADI WA UJENZI UFANYIKE KWA ORODHA NA NAMBA.

Usimamizi wa mradi wa ujenzi ni eneo lenye udhaifu mkubwa katika tasnia nzima ya ujenzi kwa ujumla, sehemu kubwa ya miradi ya ujenzi hujikuta kwenye changamoto kwa sababu ya udhaifu katika usimamizi wa ujenzi ambao unatokana na sababu mbalimbali. Udhaifu katika usimamizi wa mradi wa ujenzi ndio hupelekea makosa mengi ya kiufundi, mradi kushindwa kumalizika […]