Entries by Ujenzi Makini

MSIMAMIZI MKUU WA UJENZI ATENGENEZE MWONGOZO, UTAKAOFUATWA NA WASAIDIZI YEYE ANAPOKOSEKANA.

Mradi wa ujenzi unapokuwa katika hatua ya ujenzi huhusisha mambo mengi sana, wote tunajua kwamba karibu kila kitu kinachohusika kwenye mradi wa ujenzi ni cha muhimu sana na kinapokosewa madhara yake yanaonekana wazi na kupunguza hadhi ya jengo husika. Lakini ukitembelea eneo la ujenzi na kutathmini kazi yoyote ya ujenzi ukiwa na mtaalamu wa ushauri […]

MPANGILIO WA NGAZI NA LIFTI KWENYE JENGO.

Jengo linapomalizika kujengwa hutumiwa na watu wengi mbalimbali na aina tofauti tofauti kiasi kwamba hata aliyefanya kazi husika ya ujenzi huenda hakuwahi kuwadhania, hii ni kwa sababu matumizi yanayokuwa yamezungumzia mwanzoni huenda yakaongezeka sana zaidi ya ilivyokuwa inadhaniwa mwanzoni au hata kubadilika kabisa wakati mwingine. Hivyo kuna vitu ndani ya majengo vinapaswa kupangiliwa kwa namna […]

JENGO LA BIASHARA LAZIMA LIVUTIE KIMUONEKANO.

Kuna msemo maarufu wa kiingereza unasema “don’t judge a book by it’s cover”, ukimaanisha “usihukumu kitabu kwa muonekano wake wa nje”, sasa kama mtu hujui asili ya binadamu msemo kama huu unaweza kukupoteza ukifikiri watu huwa wanajihangaisha kufahamu undani wa kitu. Watu wengi huwa hawajihangaisha sana kufahamu undani wa kitu chochote huwa wanaishia kuhukumu kwa […]

MAKABIDHIANO KATI YA MTAALAMU ALIYEFANYA MICHORO YA RAMANI NA FUNDI AU MKANDARASI.

Imekuwa kawaida kwa watu kutafuta namna ya kukamilisha hatua ya kutengeneza michoro ya ramani kwa ajili ya ujenzi wa mradi wake wa ujenzi wakati mwingine wengine wanadiriki hata kuiba au kuchukua mitandaoni bila kujali madhara makubwa na hasara inayoambatana na kupata ramani bila kuhusika kwa mtaalamu wa usanifu. Kwa watu wengi wakishakamilisha kupata michoro ya […]

MSIMAMIZI WA MRADI WA UJENZI ANAPASWA KUWA NA ORODHA YA MAMBO ANAYOFANYIA KAZI

Ujenzi ni kazi inayohusisha vitu vingi sana katika utekelezaji wake, jambo hili unaweza kuliona ukiwa kama mtaalamu wa ushauri wa ujenzi, mkandarasi au mteja unayefanya ujenzi unapokuwa unatembelea mradi wa ujenzi. Utakuta kuna vitu vingi sana vya kutekeleza ambavyo pia vinahitaji kumbukumbu na umakini wa hali ya juu sana katika utekelezaji wake na ambavyo mara […]