Entries by Ujenzi Makini

TUMIA RAMANI ZA KWENYE MITANDAO KUONGEZA UELEWA WAKO.

Ili kufanikisha mradi wako uende kwa usahihi sana na kwa namna ambayo utaendelea kufurahia nyumba yake kwa muda mrefu zaidi baadaye unahitaji kushiriki katika kuifanya na sio kushiriki tu bali kufikiri kwa kina kujua hasa unataka kufanikisha nini katika mradi husika. Sasa mwanzoni unaweza usigundue vitu vingi muhimu unavyohitaji lakini kadiri muda unavyokwenda na kadiri […]

RAMANI ZA KWENYE MITANDAO HAZIKIDHI VIGEZO VYA KIMAMLAKA.

Kama tulivyotangulia kukubaliana kwenye makala zilizopita kwamba ramani za kwenye mitandao hazizingatia vigezo vya kiwanja ili kuja na aina sahihi ya ramani inayoendana na kiwanja husika. Hali kadhalika mamlaka husika huweka vigezo vingi ambavyo michoro inapaswa kukidhi ili uweze kupatia kibali na kuruhusiwa kujenga eneo husika, vigezo ambavyo mara nyingine hutofautiana kati ya eneo moja […]

RAMANI YA MTANDAONI HAIJATENGENEZWA KWA AJILI YAKO.

Kama nilivyotangulia kusema katika makala zilizopita kwamba kila mtu ana haiba tofauti na vipaumbele tofauti na mtu mwingine sambamba na mtazamo tofauti, matamanio tofauti, uzoefu tofauti, utamaduni tofauti, Imani tofauti na hata kipato tofauti. Haya ni mambo yanayoleta utofauti kati ya tabia ya mtu mmoja na mwingine na hata matokeo tofauti katika kazi zao. Na […]

HUWEZI KUNUNUA RAMANI YA KWENYE MTANDAO UKABAKI SALAMA.

Kazi za kitaalamu zina vitu vingi ambavyo kama ukivikiria kwa juu juu sio rahisi kuviona lakini ukija kuingia katika uhalisia ndipo unakutana navyo. Hapa kwa mfano mtaalamu wa kusanifu au kubuni jengo anatakiwa kufika katika kiwanja ambapo jengo husika linajengwa kuweza kuona ni aina gani ya jengo na kwa uelekeo gani linaweza kukaa kwa usahihi, […]

EPUKA RAMANI ZA KWENYE MITANDAO, KUTANA NA MTAALAMU.

Kabla kufikiria kuchukua ramani ya kwenye mtandao kwanza anza kufikiria ikiwa ramani husika itakuwa na changamoto au katikati ya ujenzi ukabadili mawazo na kutaka kufanya marekebisho kidogo ya ramani kabla hujaendelea, ni nani atakayekufanyia kazi hiyo ya kitaalamu? Kazi za kutoa huduma za kitaalamu ni tofauti kidogo na biashara za kuuza bidhaa ambapo ukishainunua unaweza […]