Entries by Ujenzi Makini

KAMPUNI ZA UJENZI TANZANIA ZINAPASWA KUWA NA WASHAURI WA KITAALAMU.

Wote tunafahamu kwamba nchi yetu ina uhaba mkubwa sana linapokuja suala la washauri wa kitaalamu katika sekta mbalimbali. Sekta ya ujenzi ni kati ya maeneo ambayo washauri wa kitaalamu wamekuadimika sana kwenye miradi ya ujenzi, jambo linalopelekea kushuka sana kwa ubora na thamani ya miradi ya ujenzi ukilinganisha na thamani ya fedha iliyotumika kwenye miradi […]

TENGENEZA BUSTANI NZURI KUONGEZA THAMANI YA NYUMBA NA MANDHARI YAKE.

Utengenezaji wa bustani kwa sababu za mbalimbali ikiwemo kuboresha na kupendeza mazingira ni jamba ambalo limekuwa likifanyika tangu zamani za kale. Mpangilio wa kujenga mistari ya mawe(kerbstones) na vigae vya tofali za ardhini(paving blocks) kama ardhi ngumu pamoja na upandaji miti kwa mpangilio sahihi uliotengenezwa kwenye ramani huongeza mvuto na thamani ya nyumba na mandhari […]

UNAHITAJIKA USHIRIKIANO WA WATAALAMU WOTE WANAOHUSIKA KUJENGA MRADI HUSIKA TANGU MWANZO.

Ujenzi ni kati ya miradi ambayo kukamilika kwake huhusisha taaluma nyingi za fani mbalimbali katika utekelezaji wake. Fani hizi hutegemeana sana na kuwa na madhara mbalimbali pale mpangilio sahihi wa mtiririko wa utekelezaji wa mradi husika unapokosekana. Tangu mwanzoni kabisa wa mradi watu wa fani zote husika wanapaswa kukutana na kuweka vikao ambapo kila mtu […]

KAZI NZURI INAHITAJI UMAKINI, MUDA NA UTULIVU MKUBWA.

Watu wengi kwa sababu ya kutokutafakari kwa usahihi hawajui kwa nini kazi nzuri huwa na gharama zaidi kuliko kazi ya kawaida, au kusema kwa nini kazi tofauti hutofautiana ubora na bei. Hii inapelekea watu kushindwa kuipa kazi husika uzito unaostahili na utofauti wake. Licha ya kwamba uzuri wa kazi unahitaji sana ubora, umahiri na ubobevu […]

MNG’AO KWENYE PICHA UNAOPELEKEA MNG’AO KWENYE UHALISIA NDIO MVUTO WA JENGO

Watu huvutiwa sana na muonekano mzuri unaovutia kwenye jengo bila kujua kile hasa kinachochangia wao kuvutiwa kiasi hicho na uzuri unaoonekana. Uzuri wa jengo unahusisha vitu vikubwa viwili, kimoja ni mpangilio sahihi wa vipengele vya jengo unaofuta mtiririko na uwiano unaoleta maana fulani ya kibunifu au kifalsafa na cha pili ni mng’ao wa kiwango cha […]

JENGO LINAJENGWA NA MTAALAMU(CONSULTANT), MKANDARASI NI MTEKELEZAJI TU.

Katika miradi ya ujenzi wa majengo michoro huwa inafanywa na wataalamu wa usanifu majengo pamoja na wahandisi, hawa ndio wataalamu ambao kimsingi ndio wajenzi wa jengo/mradi wenyewe. Maelekezo yote na kila kinachohusika wanakuwa wamekiwakilisha kwenye michoro kwa hiyo mkandarasi au fundi anachofanya ni kutekeleza kile ambacho kimeelekezwa kwenye michoro. Mkandarasi au fundi anapokabidhiwa michoro anatakiwa […]

JENGO LINATAKIWA KUWA NA UWIANO NA MTIRIRIKO SAHIHI

Tunapozungumzia kuhusu jengo tunazungumzia kuhusu mpangilio wa vipengele vyote vinavyounda jengo husika bila kujali kama vimepangiliwa kwa usahihi au kimakosa. Tunapozungumzia uzuri wa jengo tunazungumzia mpangilio sahihi wa vipangele vyote vya kisanifu vinavyounda jengo husika. Sasa jengo lolote lililofanyika katika viwango na lenye ubora, mvuto na lenye muonekano unaoleta maana ni lazima liwe katika uwiano […]