Entries by Ujenzi Makini

USICHOKIJUA KUHUSU KUPENDA URAHISI.

Ni asili ya binadamu kupenda vitu rahisi na vya mkato kwa sababu vinatupa unafuu wa kufanikisha jambo bila kuumia au kuteseka sana. Rahisi inashawishi kwamba unaweza kufanya jambo kubwa kwa kiasi kidogo cha rasilimali hivyo unapunguza kujihangaisha zaidi, hii ni asili ambayo ubongo ulijitengenezea tangu zamani hivyo mtu anavyosikia rahisi anasikia kupata unafuu na hisia […]

CHANGAMOTO ZA MATUMIZI YA KIWANJA

Watu wengi wamekuwa wakikutana na changamoto za kusumbuliwa na mamlaka hasa halmashauri za miji, manispaa na majiji pale wanapokuwa wanafuatilia vibali vya ujenzi kutokana na suala zima la kigezo cha matumizi ya kiwanja. Mara nyingi hasa miaka ya hivi karibuni kupata kibali cha ujenzi wa eneo lako suala la matumizi ya kiwanja limekuwa ni changamoto […]

GHARAMA ZA UJENZI ZINAJUMUISHA MICHORO YA RAMANI

Watu wengi wanapofikiria kuhusu gharama za ujenzi huanza kufikiria wakati wa kujenga, yaani kuanzia kwenye kuchimba msingi huku gharama za michoro ya ramani wakizitenganisha na ujenzi wenyewe. Jambo hili limekuwa na madhara kadhaa na limekuwa likiwaumiza wataalamu wa ujenzi na likimuumiza hata na mteja mwenyewe pia kwa sababu huwa na madhara yafuatayo. Kwa taratibu zilizowekwa […]

DAFTARI LA MAELEKEZO(INSTRUCTION BOOK)

Katika eneo la ujenzi(site) mambo huwa ni mengi sana na maamuzi yanayopelekea mabadiliko mbalimbali hufanyika mara kwa mara sana kiasi kwamba kama maamuzi hayo hayajawekwa kwenye maandishi ni rahisi baadhi ya mambo kusahaulika hivyo kutoingizwa kwenye utekelezaji kwa usahihi kama ilivyoamuliwa na matokeo yanayokusudiwa kushindwa kufikiwa. Hivyo ni muhimu sana kuwepo kwa daftari la maelekezo […]

VIKAO VYA KWENYE ENEO LA UJENZI(SITE MEETINGS)

Kwa mujibu wa taratibu zilizowekwa na mamlaka husika, kila mradi wa ujenzi hutakiwa kuwa na vikao vya mara kwa mara kwa ajili ya kujadili maendeleo ya mradi kuanzia masuala ya kiufundi ya kazi, fedha, ratiba ya kazi juu ya muda uliopangwa, mabadiliko, maamuzi mbadala pamoja na changamoto nyingine zinazoweza kuwa zinaukabili mradi husika. Vikao hivi […]

BILA KUFUATILIWA NA MSIMAMIZI MTAALAMU, KAZI YOYOTE YA UJENZI ITAHARIBIKA.

Katika kitu ambacho hutokea karibu mara zote katika mradi wa ujenzi ni pamoja na mabadiliko ya jengo wakati wa kujenga ambayo yanaleta utofauti kidogo na michoro ya mwanzo iliyokusudiwa. Mabadiliko hutokea mara zote na siku zote, wakati mwingine yakisababishwa na changamoto zilizojitokeza wakati wa ujenzi na wakati mwingine yakisababishwa na maamuzi ya mteja mwenyewe baada […]