Entries by Ujenzi Makini

VIGAE/TILES ZINAZOTENGENEZWA KWA UDONGO NA MCHANGA.

Ukiachana na vigae/tiles zinazotokana na aina tofauti tofauti za mawe na miamba zinazochimbwa kama madini na kuchongwa katika saizi tofauti tofauti kutengeneza vigae/tiles, vigae vingi vinavyotumika katika majengo vinatengenezwa katika mashine kwa mchanganyiko wa udongo wa aina tofauti tofauti na mchanga kisha kupakwa rangi na kuwekewa urembo kwa mashine ya kuchapisha. Viage hivi vinatengenezwa kwa […]

SANDSTONE OR QUARTZITE

Malighafi ya sandtone au quartzite ni aina ya mawe au miamba iliyotona na mwamba tabaka[sedimentary rocks}. Mwamba tabaka ni mwamba uliotengenezwa kutokana na mlimbikizo mkubwa wa malighafi za ardhini kama udongo, mchanga, mimea n.k., kwa mamilioni ya miaka. Sifa za Sandstone. -Haipukutiki au kumomonyoka kirahisi inapokanyagwa sana japo inategemea na namna ilivyokatwa kwa sababu iko […]

2. MARBLE, Tanzania

Malighafi ya Marble ni aina ya mawe au miamba iliyotokana na mwamba moto(metamorphic rock). Mwamba moto ni mwamba uliotengenzwa kutokana na msukumo mkubwa wa presha na joto  kali huko ndani kabisa ya ardhi ya dunia. Sifa Za Mawe au Miamba ya Marble -Marble ina uso laini na inaporomoka pale inaposuguliwa sana -Marble inaathiriwa na kemikali […]

AINA ZA MAWE ZINAZOTENGENEZA VIGAE VYA SAKAFU NA KUTA(FLOOR AND WALL TILES)

Malighafi zinazotokana na mawe hutengeneza sakafu nzuri(floor finishes) na nyingi bei zake ni nzuri pia. Malighafi zinazotokana na mawe au miamba zina faida zake nyingi ambazo hazipatikana kwa vigae(tiles) zinazotengenezwa kwa mchanganyiko wa udongo na mchanga kama vile tailizi za ceramic au porcelain. AINA ZA MALIGHAFI ZA MAWE AU MIAMBA GRANITE Aina za mawe/miamba za […]

SAKAFU YA JENGO.

Unapofikiria kumalizia sakafu ya jengo ni lazima ujiulize umalizia wake wa uso wa juu kabisa unakuwaje. -Kiwango cha utelezi; epuka kumalizia na uso wa sakafu unaoteleza sana au laini sana maeneo ya bafuni na kwenye vibarazani. -Kiwango cha upukutikaji; epuka kumalizia na uso wa sakafu unaopukutika kiurahisi kwenye maeneo yanayotumiwa wa kukanyagwa na watu wengi. […]

9. UJENZI WA JENGO KWA KUTOA NAKALA ZA 3D(3D’s PRINTING BUILDINGS)

Hii ni aina ya ujenzi ambayo mashine inaunganishwa kwenye computer ambapo mchoro wa jengo unasoma kisha zile mashine kama maroboti zinaanza kazi ya kujenga jengo husika kama vile mtu anavyotoa nakala(ku-print) maandishi ambayo yapo katika nakala tete na kutoa karatasi kwenye printer bila mtu kuigusa mashine kwa mkono. Katika ujenzi wa aina hii mashine ikishaunganishwa […]

8. UJENZI UNAOTUMIA MAROBOTI(ROBOTIC BUILDING CONSTRUCTION)

Watu mbalimbali pamoja na kampuni nyingi duniani zinaendelea kufanya na mchakato wa kutengeneza mfumo wa kutumia maroboti katika ujenzi wa nyumba. Japo hili ni jambo linalofuatiliwa na watu wengi kwa ukaribu lakini bado lina changamoto nyingi kuweza kufanikiwa kwa ufanisi unaohitajika. FAIDA ZA KUTUMIA MAROBOTI KATIKA UJENZI -Kwanza maroboti yanaweza kujenga kwa ufanisi na usahihi […]

7. (JENGO LINALOJENGWA KIWANDANI) PRE-ENGINEERING BUILDINGS

-Ujenzi wa jengo linalojengwa kiwandani ni ile hali ya mkandarasi kwenda kufanyia ujenzi wake kiwandani kisha kulisafirisha mpaka saiti eneo na kulifunga. Tofauti ya ujenzi unaonzia kiwandani na jengo linaloanzia kiwandani ni kwamba ujenzi unaoanzia kiawandani mkandarazi anaweza kuagiza atengenezewa kitu cha umbo fulani kiwandani kisha kupelekewa saiti lakini jengo linaloanzia kiwandani mkandarasi mwenyewe ndio […]

6. UJENZI UNAONZIA KIWANDANI(PRECAST CONCRETE CONSTRUCTION)

Ujenzi unaoanzia kiwandani ni aina ya ujenzi ambao vifaa vya ujenzi vinatengenezewa eneo jingine tofauti na eneo jengo linapojengwa. Vifaa vikishatengenezwa vinasafirishwa kwenda eneo la ujenzi kisha kufungwa. Hii ni tofauti na ujenzi wa kawaida ambao kila kitu kinafanyikia eneo jengo linapojengwa. FAIDA ZA UJENZI UNAONZIA KIWANDANI Ujenzi unaonzia kiwandani hurahisisha kazi ya ujenzi kama […]

5. UJENZI WA JENGO LINALOBEBWA NA KUTA

5. UJENZI WA JENGO LINALOBEBWA NA KUTA Hii ni aina ya ujenzi ambayo imetumika sana kwa majengo ya ghorofa miaka ya 1700 mpaka 1900 mzigo wote wa jengo unabebwa na kuta za jengo badala ya nguzo na boriti(beams). Siku hizi aina hii ya ujenzi haitumiki tena isipokuwa kwa majengo madogo ya makazi na ni kwa […]