Entries by Ujenzi Makini

CHANGAMOTO ZISIZOTARAJIWA KWENYE UJENZI.

Moja kati ya changamoto kubwa ambayo mara nyingi huwa tunakutana nayo kwenye ujenzi ni kukutana na changamoto usiyoitarajia. Changamoto zisizotarajiwa hutokea wakati wowote na kuleta usumbufu mkubwa na wakati mwingine hata hasara kwa sababu inaweza kuwa ni changamoto ambayo utatuzi wake unakuwa sio rahisi. Changamoto hizi tunapokutana nazo zinayumbisha sana mradi wa ujenzi kwa sababu […]

MLIMA KAMA KAZI KATI YA MTAALAMU ALIYEFANYA MICHORO YA RAMANI NA FUNDI AU MKANDARASI.

Imekuwa kawaida kwa watu kutafuta namna ya kukamilisha hatua ya kutengeneza michoro ya ramani kwa ajili ya ujenzi wa mradi wake wa ujenzi wakati mwingine wengine wanadiriki hata kuiba au kuchukua mitandaoni bila kujali madhara makubwa na hasara inayoambatana na kupata ramani bila kuhusika kwa mtaalamu wa usanifu. Kwa watu wengi wakishakamilisha kupata michoro ya […]

GHARAMA YA UJENZI ULIOPEWA NI MAKADIRIO TU.

Unaweza kufurahia au kuumizwa na gharama ya ujenzi uliopewa kwa kuiangalia kwa sababu umeamini kwamba hiyo ndio gharama inayokwenda kumaliza kazi yako. Nachopenda kukushauri ni kwamba hutakiwi kufurahia wala kuumizwa na gharama ya ujenzi unayopewa na fundi au mkandarasi kwa ajili ya kukujengea jengo lako kwa sababu kwa sehemu kubwa hiyo sio gharama halisi. Na […]

UJENZI NI UTAALAMU NA UZOEFU.

Moja kati ya changamoto ambayo huwakuta wataalamu waliomaliza chuo siku za karibuni na kuingia kwenye kazi za ujenzi ni pamoja na kuwa na uwezo mdogo kwenye kazi za ufundi wa ujenzi. Suala la wataalamu wa ujenzi kuwa na uwezo mdogo katika shughuli za ujenzi haliwaathiri vijana waliotoka chuoni peke yake bali hata wataalamu wakongwe ambao […]