Entries by Ujenzi Makini

UJENZI UNATAKA UTAALAMU NA UZOEFU.

Kati ya vitu ambavyo vimekuwa vikinishangaza sana kwa muda mrefu ni jinsi kwamba kila mradi wa ujenzi unapofanyika huwa kuna makosa yanafanyika na kutakiwa kurekebishwa na kwa kutumia mtaalamu mwenye uzoefu bila kujalisha kuna fundi mjenzi mwenye uzoefu wa miaka mingapi katika utekelezaji wa mradi huo. Yaani hata unapokuta kuna umakini kiasi gani katika eneo […]

CHANGAMOTO MPYA KWENYE UJENZI ZITUMIKE KUUBORESHA MFUMO.

Kama tulivyoendelea kujadili kwenye makala zilizopita njia nzuri ya kupunguza makosa kwenye miradi ya ujenzi ni kuwa na mchakato maalum unaofuatwa hatua kwa hatua katika utekelezaji wa mradi wa ujenzi. Mfumo huo unatumika badala ya kutegemea maamuzi ya mtu au msimamizi mmoja ambaye ndiye anatoa maelekezo yote badala yake mchakato mzima wa utekelezaji unakuwa upo […]

UJENZI WA NYUMBA KIJIJINI.

Watu wengi hasa katika nchi zinazoendelea ni aidha wa wametokea vijiji au wazazi wao walitokea vijijini hivyo wana makazi ya kurithi katika maeneo ya vijijini. Sasa kutokana na uhalisia huo watu wengi wamekuwa wakisukumwa kujenga nyumba za kuishi katika maeneo waliyotokea hata kama hawaishi maeneo haya kwa muda wote wakiwa na sababu mbalimbali. Kuna wengine […]

MRADI WA UJENZI USIOENDESHWA KWA MFUMO.

Kabla ya kujadili namna ya kuendesha mradi wa ujenzi bila mfumo au pamoja na mfumo kwanza tujadili mfumo ni nini? Mfumo maana yake ni utaratibu fulani uliopangwa ambao unafuata mchakato maalum katika ufanyaji wa mambo yake kwa kufuata mfululizo fulani uliopangiliwa. Mchakato unaofuatwa katika mfumo husika mara nyingi huwa na hatua au vitendo vinavyojirudia rudia […]

CHANGAMOTO YA KUKOSEKANA KWA MSANIFU MAJENGO KWENYE MRADI WA UJENZI.

Kama tulivyojadili mara nyingi sana katika makala zilizopita kwamba kuna mapungufu mengi sana hujitokeza katika miradi ya ujenzi kwa sababu ya kukosekana kwa wataalamu husika wa ujenzi huo. Ikiwa mtaalamu kamili hatatumika kuanzia hatua ya michoro mpaka mwisho basi jengo litakuwa na mapungufu makubwa sana kuanzia ya kimatumizi mpaka kimuonekano. Na ikiwa mtaalamu atahusika katika […]

KAZI YA UBUNIFU YA USANIFU WA MAJENGO INAFANYIKA KWA VITENDO.

Mahitaji ya wateja katika miradi ya usanifu au ubunifu majengo yamekuwa yakipatikana kupitia majadiliano katika mteja au wateja na washauri wa kitaalamu katika ubunifu majengo wakati mwingine sambamba na uhandisi majengo. Hilo ni jambo sahihi kabisa kwa sababu hiyo ndio namna pekee ambapo mteja anaweza kupata kile hasa ambacho anakitazamia na kukitegemea kwa kuwa kwa […]

MRADI WA UJENZI UNAHITAJI MAANDALIZI MAKINI SANA KABLA ILI KUEPUKA USUMBUFU BAADAYE.

Ni wazi kwamba kwa mtu yeyote ambaye amewahi kujenga na kusimamia ujenzi wake mwenyewe anajua ni jinsi gani mradi wa ujenzi unavyoambatana na changamoto na usumbufu mkubwa wakati wa utekelezaji wake hasa kama hakukuwa na maandilizi na mikakati madhubuti mwanzaoni. Katika usumbufu huu kitu ambacho hugharimu sana ni muda ambao mradi huo unachukua katika kufuatilia […]