Entries by Ujenzi Makini

KUNA NAMNA NYINGI ZA KUIBORESHA NA KUIREKEBISHA NYUMBA YAKO YA SASA KUWA YA KISASA ZAIDI.

Maboresho na ukarabati ni kati ya vitu ambavyo ni muhimu sana katika nyumba ambayo imeshatumika kwa miaka kuanzia mitano na kuendelea kwa sababu mambo mengi yanaenda yakibadilika kila siku na hivyo vifaa na teknolojia inabadilika pia hivyo kufanya mabadiliko ni jambo muhimu la kufikiria na kuzingatia. Lakini pamoja na hayo mara nyingi wakati tunajenga nyumba […]

ENEO LA UJENZI HALITAKIWI KURUHUSIWA MTU ASIYEHUSIKA KUINGIA.

Mamlaka na taasisi zinahusika na mambo mbalimbali usalama katika maeneo ya kazi zimeainisha mazingira na taratibu mbalimbali za kazi katika maeneo husika. Taratibu hizi licha ya kwamba huwa hazifuatwa kwa uhakika na wakati mwingine zinapuuzwa sana lakini zimewekwa kwa kuzingatia mambo mbalimbali na yote yakiwa na lengo na umihumu fulani. Moja kati ya taratibu zinazojulikana […]

KILA NYUMBA/JENGO LINA GHARAMA YAKE TOFUATI.

Jambo ambalo huwa tunakutana nalo kila siku na timu yetu hapa ofisini ni watu mbalimbali hususan wanaopitia katika tovuti hii na kwingine kuuliza gharama mbalimbali za kazi za ujenzi walizokutana nazo kwenye tovuti au maeneo mengine. Hii inatokana na kwamba watu hudhani nyumba yao au mradi wao wa ujenzi unaenda kuwa kile wanachokiona na kwamba […]

KIKAO CHA KWANZA KABLA YA MRADI WA UJENZI KUANZA NI MUHIMU SANA.

Siku za hivi karibuni kuna ujenzi wa nyumba moja kubwa ya kuishi umekuwa unaendelea, sasa mradi huo unasimamiwa na msimamizi wa ujenzi peke yake(foreman) ambaye ndiye anahakikisha utekelezaji unazingatia kila kilichofanyika kwenye michoro. Kazi hiyo ya michoro nimeifanya mwenyewe lakini kwenye usimamizi huwa nafika eneo la ujenzi mara chache hivyo sehemu kubwa ya maamuzi madogo […]

KWENYE UJENZI UNAWEZA KUTUMIA MALIPO KUHAKIKISHA UBORA WA KAZI.

Kumekuwepo na changamoto kubwa sana kwenye suala la ufanyaji kazi na hasa kufanya kazi katika viwango bora na kwa usahihi. Changamoto za kufanya kazi isiyo katika viwango bora(poor workmanship) inachangiwa na sababu mbalimbali kama vile kushindwa kuweka vipaumbele kwa usahihi, malipo duni, kukosekana usimamizi na ufuatiliaji makini n.k., Lakini hata hivyo pamoja na changamoto zote […]

KWENYE UJENZI USIPOJUA SEHEMU SAHIHI YA KUCHUKUA USHAURI UTAINGIA KWENYE MAJUTO.

Ikiwa mtu unahitaji kupata ushauri wa uhakika ambao utakuwa na majuto kidogo katika masuala yote yanayohusiana na ujenzi ni muhimu sana kuwa na mtaalamu mshauri wa masuala ya ujenzi ili kuepuka kuchukua ushauri kwa watu wasio sahihi ambao utakufanya ufanye maamuzi yatakayokuja kukugharimu sana baadaye. Kila mtu anajua umuhimu wa utaalamu katika fani yoyote ile […]