Entries by Ujenzi Makini

UJENZI NI MAHESABU

Kwa mtu ambaye una mpango wa kujenga ndani ya kipindi cha chini ya miaka mitano ijayo, jambo la kwanza na muhimu unalotakiwa kufanya kwa sasa ni kuanza mchakato. Kadiri unavyoanza mchakato mapema ndivyo kadiri na kufahamu mambo mengi mapema ndivyo unavyopunguza makosa na kurahisisha zoezi hilo. Unaweza kujiuliza unaanzaje mchakato wakati bado huoni pa kuanzia, […]

KARIBU KWA USHAURI WA KITAALAMU JUU YA UJENZI

Jambo la kwanza kabisa unalopaswa kufikiria unapotaka kujenga linapaswa kuwa unapata wapi mtaalamu wa kukushauri juu ya ujenzi wa mradi wako kadiri ya hali yako ilivyo kwa ujumla na kile unacholenga kufanikisha. Kupata ushauri sahihi wa kitaalamu mara nyingi kutakuepusha na majuto mbeleni pamoja na hasara ambayo wakati mwingine inaweza kuwa kubwa sana. Uzuri ni […]

KUBADILISHA MATUMIZI YA KIWANJA UNAHITAJI MICHORO YA RAMANI.

Viwanja katika maeneo mbalimbali vimepangiwa matumizi na wataalamu wa mipango miji katika wizara ya ardhi kwa namna ambayo wanaona ni sahihi zaidi kitaalamu. Lakini hata hivyo wizara imetoa uhuru wa mtu kuamua kufanya mabadiliko ya matumizi kadiri ya namna alivyoamua kutumia kiwanja chake. Uhuru wa mtu kufanya mabadiliko ya matumizi ya kiwanja umewekwa kwa sababu […]

KUBADILI MATUMIZI YA KIWANJA

Changamoto kubwa sana ambayo watu wamekuwa wakikutana nayo mara kwa mara wanapokuwa wanashughulika na kibali cha ujenzi ni suala la matumizi ya kiwanja. Eneo la matumizi ya kiwanja limekuwa ndio eneo linaloongoza kwa kukwamisha miradi mingi zaidi ya ujenzi. Changamoto iliyopo ni kwamba eneo la matumizi ya kiwanja lina vipengele vingi sana ambavyo vimegawanyika katika […]