Entries by Ujenzi Makini

KUJENGA KWA HATUA NI BORA KULIKO KUCHAKACHUA GHARAMA.

Watu wengi wanapofikia hatua ya kuamua kuanza ujenzi wakiwa tayari wameweka kiasi cha fedha ambacho walitegemea kingefanikisha kukamilisha mradi mzima wa ujenzi mara nyingi wanakuta fedha hiyo haitoshi na wanahitajika fedha zaidi pengine nyingi sana ukilinganisha na iliyopo. Sasa inapotokea watu wanapojikuta katika hali hii baadhi huamua kufikiria namna ya kupunguza gharama za ujenzi ziendana […]

MAENEO 9 YA USIMAMIZI KATIKA USIMAMIZI WA JUMLA WA MRADI WA UJENZI(PROJECT MANAGEMENT)

Wote tunakubaliana kwamba shughuli yoyote ya ujenzi inaweza kufanyika kwa viwango vya juu vya ubora au kwa viwango vya chini vya ubora kutegemeana na uwezo wa kiusimamizi(project management). Sasa usimamizi sahihi na kamili wa ujenzi unahusisha maeneo haya tisa. Usimamizi wa kuunganisha shughuli zote za ujenzi ziende katika utaratibu sahihi uliopangwa kwa ajili ya kufanikisha […]

USIMAMIZI WA MRADI WA UJENZI UFANYIKE KWA ORODHA NA NAMBA.

Usimamizi wa mradi wa ujenzi ni eneo lenye udhaifu mkubwa katika tasnia nzima ya ujenzi kwa ujumla, sehemu kubwa ya miradi ya ujenzi hujikuta kwenye changamoto kwa sababu ya udhaifu katika usimamizi wa ujenzi ambao unatokana na sababu mbalimbali. Udhaifu katika usimamizi wa mradi wa ujenzi ndio hupelekea makosa mengi ya kiufundi, mradi kushindwa kumalizika […]

MKOPO WA NYUMBA(MORTGAGE)

Mara kwa mara watu wamekuwa wakiniuliza endapo wanaweza kupata aina ya mkopo wanaoweza kuumudu kwa ajili ya kuendeleza eneo la ujenzi alilonalo au hata kupata mwekezaji ambaye wanaweza kuingia ubia wa pamoja waweze kuendeleza eneo kwa kujenga jengo la biashara kwa makubaliano yenye manufaa kwa pande zote mbili. Japo mikopo ya nyumba ipo ya aina […]

RANGI ZA JENGO.

Mpangilio wa rangi katika jengo ni kati ya vipengele vya ujenzi vyenye utata na vinavyoleta wakati mgumu sana katika kuchagua mpangilio sahihi. Japo kuna watu wataalamu na wabobezi kwenye masuala ya mpangilio wa rangi lakini suala la rangi mara nyingi kila mtu huwa na ladha yake tofauti anayoipenda au kuvutiwa nayo na mara nyingi huwa […]