Entries by Ujenzi Makini

FIKIRI KWA USAHIHI KUPUNGUZA GHARAMA ZA UJENZI.

Kawaida gharama za ujenzi wa nyumba mpaka inakamilika huwa ni kubwa, kwa ujumla kujenga nyumba sio kitu unaweza kukilinganisha na vitu kama kununua gari au kununua kiwanja kwani gharama za ujenzi ni kubwa sana mpaka nyumba kukamilika. Ukubwa wa gharama hizi umekuwa ukiwafanya watu kufikiria sana namna ya kuzipunguza kwa njia mbalimbali na hapa ndipo […]

MICHORO YA RAMANI KUCHELEWA KUKAMILIKA.

Wateja wengi wamekuwa wakishangazwa na kwa nini kazi ya michoro inachukua muda mrefu sana kukamilika tofauti na matarajio yao na saa nyingine hasa kuvuka ile tarehe ya makubaliano kwamba michoro itakuwa tayari. Kuna sababu mbalimbali ambazo hupelekea michoro kuchelewa, nyingine zikiwa sababu za msingi kidogo lakini nyingi zikiwa sio sababu za msingi kwa michoro kuchelewa. […]

UJENZI WA HARAKA UNAOZINGATIA MUDA NA WENYE UBORA

Kuna miradi ya ujenzi ambayo huwa inahitajika kufanyika kwa haraka yaani kwa muda mfupi iwe imekamilika kwa sababu aidha ni ya dharura au inahitajika haraka kwa sababu nyingine yoyote iweze kukabidhiwa ndani ya muda mfupi sana lakini ikiwa kwenye ubora wa hali ya juu. Huu ni ujenzi ambao kwa mfano nyumba ya ghorofa moja kwenda […]

MAPATANO YA BEI YA RAMANI NA KUJENGA YAWE NA MSINGI

Imekuwa ni changamoto sana kwa watu kupata uhakika kama gharama wanazolipa na kulipwa kwa huduma za ujenzi wanazotoa ni kiwango sahihi ama ni kubwa sana au ndogo sana. Hili wakati mwingine limekuwa likipelekea kukosekana kuridhika kwa pande hizo mbili na kwa kiasi fulani kuathiri ubora wa kazi pia. Jambo hili limekuwa likichangiwa na kukosekana na […]

MAMBO YA KUZINGATIA IKIWA UNATAKA KUJENGA NYUMBA YENYE “BASEMENT FLOOR” KATIKA ENEO LENYE MWINUKO/MTEREMKO MKALI.

Jambo la kwanza na muhimu la kuzingatia ikiwa unataka kujenga nyumba yenye ghorofa inayoanzia chini ardhini maarufu kama “basement floor” katika eneo lenye mteremko mkali ni kina chake au ukali wa mteremko wenyewe. Wapo watu ambao wakishaona eneo lake lina mwinuko kidogo tu anataka kuweka ghorofa inayoanzia chini ardhini, lakini ukweli ni kwamba sio kila […]

KUJENGA KWENYE ENEO LENYE MWINUKO/MTEREMKO.

Watu wengi wanaomiliki viwanja kwenye maeneo yenye mwinuko au mteremko mkali hujaribu kufikiria namna zaidi ya kutumia kiwanja chake husika kwa namna sahihi zaidi kadiri ya umbo ambalo kiwanja chake kinachukua. Maeneo yenye mwinuko ni maeneo mazuri sana katika kufanikisha ujenzi wa jengo lenye kuvutia na linaloonekana vizuri na kwamba usahihi. Watu wengi huamua kwamba […]

UBORA WA KAZI YA UJENZI HAUTOKEI KWA BAHATI MBAYA.

Ni sheria ya asili kwamba hakuna kitu kizuri na chenye ubora kinachoweza kutokea bila kuweka juhudi kubwa za makusudi na maarifa muhimu yaliyohusisha uzoefu wa hali juu katika kufanikisha jambo husika. Changamoto zinazojitokeza katika kila jambo bora linalofanyika ni nyingi sana na zinahitaji maarifa na kazi kubwa kukabiliana nazo na kupelekea matokeo bora yanayotarajiwa kutofikiwa […]