Entries by Ujenzi Makini

KUFANIKISHA UJENZI BORA EPUKA KUTUMIA HISIA, ANGALIA MANUFAA.

Mara nyingi sisi binadamu tuna udhaifu wa kuongozwa na hisia zaidi na kutoona uhalisia jambo linalopelekea kufanya maamuzi yasiyo sahihi mara nyingi zaidi kuliko maamuzi sahihi na mwishoni tunaishia kujutia na kusema laiti ningejua, watu wachache ambao wamejaliwa kutumia akili na maarifa zaidi kuliko hisia wamekuwa wanashinda zaidi kuliko wengi wanaoongozwa na hisia. Changamoto ni […]

KUEPUSHA KUHARIBU KAZI, MPE MTAALAMU UHURU WA KUTOSHA

Mara nyingi kama wewe ni mteja mtaalamu wa kufanya jengo huwa anakusikiliza unataka nini na kufanya unachotaka kwa sababu lengo lake ni kukuridhisha wewe na kufanya unachotaka kwa sababu wewe ndiye unayelipa pesa na mwisho wa siku wewe ndiye mmiliki wa jengo husika. Changamoto huwa inatokea pale mteja ndio anakuwa mpangaji na mwamuzi wa kila […]

UKUBWA WA NYUMBA UNATOKANA NA UKUBWA WA VYUMBA NDANI YA NYUMBA

Imekuwa kawaida kukutana na mteja anakwambia nahitaji nyumba iwe na vyumba vikubwa ndani vyenye ukubwa wa kutosha, anakwambia “nataka sebule kubwa na master bedroom kubwa” lakini mwisho anaishia kukwambia lakini nyumba yenyewe isiwe kubwa, kwa sababu anataka nyumba ambayo haitamgharimu sana fedha nyingi kuijenga. Kwanza kabisa nakubali kwamba kadiri nyumba inavyokuwa kubwa ndivyo kadiri gharama […]

KUDHIBITI UBORA WEKA MSIMAMIZI WA NJE KWENYE MRADI WAKO WA UJENZI.

Kwenye miradi mikubwa ya ujenzi ambayo hufuata taratibu zote zilizowekwa mambo mengi huwekwa kwenye maandishi ikijumuisha viwango ambavyo vinategemewa kufikiwa, hata mikataba ya miradi hii huingiwa kwa masharti ambayo yanalazimisha kila kitu kilichopangwa kufikiwa katika viwango vilipangwa na kwa mategemeo ya mteja. Lakini inapokuja kwenye miradi midogo au miradi mikubwa lakini haijafuata taratibu sahihi zilizopangwa […]

USIOKOTOZE RAMANI UKAJENGA, TAFUTA MTAALAMU

Kuokotoze ramani na kisha kuijenga ni kutokuthamini kile unachokwenda kujenga licha ya kwamba unatumia mamilioni ya pesa kujenga. Inashangaza sana kwamba unakuta mtu anaenda kujenga nyumba ya milioni 90 lakini naokoteza ramani au anatafuta ramani ambayo imetumiwa na mtu mwingine wakati gharama ya kutumia mtaalamu kwa huduma yote ya ushauri pamoja na michoro labda ni […]

UNACHOHITAJI KUTOKA KWA MTAALAMU WA USANIFU MAJENGO(ARCHITECT) KWA AJILI YA KUANZA MRADI WA UJENZI.

Kama nilivyotangulia kusema katika makala zilizopita, usijaribu kujenga nyumba kabla ya kuonana na mtaalamu wa usanifu majengo(Architect) akupe mwongozo mzima wa kitaalamu sambamba na vigezo na masharti vilivyowekwa na mamlaka husika vinapaswa kufikiwa ili kupata kibali cha kuendelea na ujenzi, ukiendelea bila ushauri wa kitaalamu kuna nafasi kubwa sana kwamba unatafuta majuto mbeleni. Kuweza kupatiwa […]