Entries by Ujenzi Makini

KUDHIBITI UBORA WEKA MSIMAMIZI WA NJE KWENYE MRADI WAKO WA UJENZI.

Kwenye miradi mikubwa ya ujenzi ambayo hufuata taratibu zote zilizowekwa mambo mengi huwekwa kwenye maandishi ikijumuisha viwango ambavyo vinategemewa kufikiwa, hata mikataba ya miradi hii huingiwa kwa masharti ambayo yanalazimisha kila kitu kilichopangwa kufikiwa katika viwango vilipangwa na kwa mategemeo ya mteja. Lakini inapokuja kwenye miradi midogo au miradi mikubwa lakini haijafuata taratibu sahihi zilizopangwa […]

USIOKOTOZE RAMANI UKAJENGA, TAFUTA MTAALAMU

Kuokotoze ramani na kisha kuijenga ni kutokuthamini kile unachokwenda kujenga licha ya kwamba unatumia mamilioni ya pesa kujenga. Inashangaza sana kwamba unakuta mtu anaenda kujenga nyumba ya milioni 90 lakini naokoteza ramani au anatafuta ramani ambayo imetumiwa na mtu mwingine wakati gharama ya kutumia mtaalamu kwa huduma yote ya ushauri pamoja na michoro labda ni […]

UNACHOHITAJI KUTOKA KWA MTAALAMU WA USANIFU MAJENGO(ARCHITECT) KWA AJILI YA KUANZA MRADI WA UJENZI.

Kama nilivyotangulia kusema katika makala zilizopita, usijaribu kujenga nyumba kabla ya kuonana na mtaalamu wa usanifu majengo(Architect) akupe mwongozo mzima wa kitaalamu sambamba na vigezo na masharti vilivyowekwa na mamlaka husika vinapaswa kufikiwa ili kupata kibali cha kuendelea na ujenzi, ukiendelea bila ushauri wa kitaalamu kuna nafasi kubwa sana kwamba unatafuta majuto mbeleni. Kuweza kupatiwa […]

SIFA ZA RAMANI SAHIHI YA JENGO

Wateja wengi wamekuwa wanakutana na changamoto sana linapokuja suala la ramani iliyokidhi vigezo vya kuitwa ramani bora ya jengo au ramani sahihi ya jengo na kwa sababu wateja wengi ni watu wasio na uzoefu kwenye fani hizi za usanifu na uhandisi basi sio rahisi kuona makosa yanayokuwepo kwenye ramani hizi mpaka jengo linapohamiwa ndipo huja […]

UBORA WA RAMANI YA JENGO.

Nini maana ya ubora wa ramani ya jengo? Ramani ya jengo yenye ubora ni ramani ambayo imefanyika kwa usahihi unaohutajika kwa maana ya kwamba ni ramani inayozingatia viwango sahihi kwenye kila eneo kuanzia vipimo sahihi, uelekeo sahihi, mpangilio sahihi wa kimatumizi, mpangilio sahihi wa vitu vinavyoamua uzuri wa muonekano wa jengo husika, mapendekezo sahihi ya […]

MUDA NI FEDHA, KASI NI THAMANI.

Kadiri kitu kinavyoweza kufanyika kwa haraka zaidi lakini kwa ubora ule ule gharama ya kukikamilisha huwa inakuwa kubwa zaidi kuliko kinapofanyika kwa kutumia muda mrefu zaidi. Mfano mzuri ni kwenye usafiri, kwamba pamoja na mambo mengine kama vile usalama na mazingira bora ya ndani ya chombo cha usafiri, lakini usafiri unaowahi zaidi huwa na gharama […]