Entries by Ujenzi Makini

KULINDWA NA SHERIA KWENYE UJENZI FANYA KAZI NA KAMPUNI KWA MKATABA EPUKA MAFUNDI.

Kisaikolojia binadamu wengi tunapenda sana urahisi, sio tu urahisi wa gharama bali hata urahisi wa michakato na urahisi wa kukamilisha jukumu husika. Kweli japo ubongo unatupeleka kwenye kutafuta urahisi kwa manufaa fulani lakini hilo mara nyingi huambatana na gharama kubwa sana. Watu wengi linapokuja suala la ujenzi mara nyingi hutafuta watu wa kawaida au mafundi […]

CHANGAMOTO ZA USIMAMIZI WA MRADI WA UJENZI.

Watu wengi kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kudhibiti na kujaribu kupunguza gharama huchagua kusimamia miradi yao ya ujenzi wenyewe. Hakuna ubaya wowote kwenye kusimamia mradi wako wa ujenzi mwenyewe na kimsingi itakusaidia sana katika kuuelewa vizuri ujenzi ambao wengi hawauelewi. Na zaidi ya hapo ni kwamba kama utakuwa makini vizuri na kutumia akili sana kusimamia […]

UNAHITAJI KUANZA MCHAKATO WA MRADI WAKO WA UJENZI SASA HIVI.

Watu wengi wana mtazamo kwamba watakuja kuanza kushughulika na miradi yao ya ujenzi wakati fulani muda ukifika. Labda wakishapata fedha au wakishanunua kiwanja/eneo wanalokwenda kujenga au labda wakishaanza mradi fulani ambao utakwenda kuwaletea pesa. Swali ni je, ni upi wakati sahihi kwako kuanza mradi wako wa ujenzi? Wakati sahihi wa kuanza mradi wako wa ujenzi […]

NANI ANAKUWEPO KATIKA ENEO LA UJENZI MUDA WOTE?

Kumekuwepo na maswali mengi na sintofahamu kubwa juu ya uwepo wa wataalamu kwenye eneo la ujenzi wakati wote. Hili limekuwa likileta sana pia maswali kwa watu wengi ambao hawaelewi juu ya wasimamizi wa ujenzi ni nani na anayekuwepo katika eneo la ujenzi muda wote ni nani. Kimsingi kabisa mtu ambaye unampata katika eneo la ujenzi […]

GHARAMA ZA UJENZI HAZIKO KWENYE TOFALI.

Imekuwa ni jambo la kawaida kwa binadamu walio wengi kuhukumu vitu kwa kuangalia jinsi vinavyoonekana kwa nje. Muonekano umekuwa ndio kipimo cha vitu kwa sababu ya watu kutokuwa na uelewa wa haraka juu ya undani wa mambo mbalimbali. Hivyo watu wamekuwa wakipima kila kitu wasichokijua kiundani kutokana na muonekano wake. Jambo hilo halijaenda tofauti sana […]

GHARAMA ZA UJENZI NI ZILE ZILE.

Ukishakuwa ni mtu unayehusika na mambo ya ubunifu, usanifu na uhandisi wa majengo basi unapotembea kila mahali hususan kwenye miji mikubwa na kwenye makazi ya watu macho siku zote yanaangalia mazingira yanavyojengwa na aina mbalimbali za ubunifu uliofanyika. Katika kufanya hivi mtu unaweza kuona jinsi kuthamini na kulipia utaalamu kunavyoendelea kuongeza thamani ya majengo na […]