UJENZI NA RAMANI
Architect Sebastian Moshi. Whatsapp/Call Asingejaribu kuokoa
This author has not written his bio yet.
But we are proud to say that Ujenzi Makini contributed 773 entries already.
Architect Sebastian Moshi. Whatsapp/Call Asingejaribu kuokoa
Kama nilivyotangulia kusema kwenye makala zilizopita linapokuja suala la ujenzi basi tabia ya uaminifu kwa fundi au mkandarasi anayepewa kazi ni jambo la lazima ikiwa unahitaji mradi wa ujenzi umalizike vizuri na kwa amani bila mivutano na ubabaishaji. Lakini changamoto ni kwamba tabia ya uaminifu ndio tabia adimu zaidi katika tabia za watu, inachukua muda […]
Mamlaka mbalimbali za serikali pamoja na nyingine zisizo na uhusiano wa moja kwa moja na serikali zimeendelea kuboreshwa na kutanuka zaidi katika kuwapelekea watu huduma karibu sana na wao ili pia kuweza kudhibiti mambo yafanyike kwa kufuata utaratibu uliowekwa. Kutokana na kutanuka sana kwa mamlaka hizi basi watu wengi sana siku wanajitahidi kujiongeza kwa kufuatilia […]
Kuna maswali huwa najiuliza kuhusu namna ujenzi unafanyika na yananiletea tena maswali zaidi. Watu wengi huwapa watu au makampuni mbalimbali kazi za kuwajengea majengo yao au nyumba zao mkataba wa jumla kwa maana ya kusambaza vifaa na ufundi kwenye jengo au kwa maana ya kila kitu kwa imani waliyoijenga kwao lakini wengi hawana mfumo au […]
Kutoka kwenye uzoefu wa watu wengi sana niliokutana nao mara nyingi watu huanza miradi yao ya ujenzi wakiwa hawana uhakika kama wanakwenda kukamilisha miradi hiyo na huanza kama utani tu wakiwa hawajui ni lini watakamilisha miradi yao. Lakini kwa sababu baada ya mtu kuanza huweka nguvu na akili zake zote kwenye mradi huo wa ujenzi […]
Kwa muda sasa nimekuwepo kwenye hii tasnia ya ujenzi kwa maeneo yote kuanzia kwenye eneo la ushauri wa kitaalamu na michoro ya ramani mpaka kwenye eneo la usimamizi wa ujenzi na kujenga nimejifunza mambo mengi mbalimbali. Kiuhalisia mambo ya kujenga kwenye ujenzi ni mengi sana na huwa hayaishi, na pale unapodhani kwamba umeshajua kila kitu […]
Watu mbalimbali huwa wanapewa nyumba za urithi au kununua eneo ambalo tayari kuna nyumba ndani yake hivyo anakuwa amenunua eneo hilo pamoja na nyumba hiyo. Baada ya uwezo wa kifedha kuongezeka na shauku ya kujenga nyumba bora nzuri na ya kisasa kujenga hamasa huamua kubomoa nyumba hiyo ili kujenga nyumba nyingine mpya kabisa eneo hilo. […]
Kwa maeneo ya mjini sasa ni wazi kwamba muamko wa watu kufuatilia vibali vya ujenzi kwa majengo na nyumba zao umekuwa mkubwa sana. Watu wengi sasa kila wanapofikiria kuhusu kujenga kwenye maeneo ambayo yako chini ya halmashauri za miji, manispaa na majiji wamekuwa wanafikiria kwanza kuhusu kibali cha ujenzi na hata usajili wa kwenye mamlaka […]
Kwa miaka ya siku hizi sehemu kubwa ya ardhi iliyopo ndani ya halmashauri za miji/manispaa/majiji zimepimwa au tayari kuna ramani ya kiwanja kwa ajili ya matumizi mbalimbali hususan makazi. Kazi hii ya upimaji sio kazi inayofanywa kiholela au kiurahisi tu na mtu yeyote bali ni kazi ya kitaalamu inayofanywa na watu wenye taaluma husika wanaofahamika […]
Mara nyingi katika kazi tunazofanya tumekuwa tunakutana na wateja ambao wanahitaji kufanyiwa kazi za michoro ya ramani kisha baada ya hapo wanahitaji kufanyiwa kazi za ukadiriaji wa gharama za ujenzi wa majengo ambapo wanategemea wewe mwenyewe ndio ufanye kazi hiyo. Licha ya kwamba ni kweli kwamba mtaalamu wa usanifu majengo au uhandisi mihimili anaweza kupitia […]
Ujenzi Makini ni Mtandao unaotoa elimu na ushauri kwa mambo yote yanayohusu ujenzi na changamoto zote za kiufundi na kitaaluma katika fani ya ujenzi kwa lengo la kuboresha zaidi huduma na mazingira ya ujenzi kwa ujumla.
Dar es Salaam, Tanzania.
+255 717 452 790
info@ujenzimakini.com