Entries by Ujenzi Makini

UTAALAMU WA KUCHORA NA KUJENGA NYUMBA YOYOTE NDIO UNAOTUMIKA KWENYE KUCHORA NA KUJENGA NYUMBA/JENGO LINGINE LOLOTE.

Mara kwa mara nimekuwa nikikutana wateja mbalimbali wenye mahitaji tofauti tofauti ya kila namna. Licha ya kwamba mahitaji haya yamekuwa yakija kwa upekee tofauti tofauti kuna kitu kimoja kimekuwa kikinishangaza na kuleta usumbufu kidogo. Jambo hilo ni wateja kuamini kwamba mtalaamu anatakiwa awe alishafanya jengo la aina fulani ili kuwaza kufanya mradi wake huo. Ingawa […]

KWENYE UJENZI USIPOKEE USHAURI AMBAO HUJAOMBA.

Kwa asili sisi binadamu tuna tabia ya kisaikolojia ya kurithi ambapo huwa tunawamaamini zaidi watu wetu wa karibu au watu ambao tuna mahusiano nao ya karibu kuliko watu wa mbali tusiowajua au kuwa na ukaribi nao. Yaani tumeumbwa kwamba wale watu ambao tuna mahusiano ya karibu na ya kina huwa tunaamini zaidi kile wanachotuambia na […]

KUONGEZA THAMANI YA JENGO KATIKA HATUA YA UJENZI.

Changamoto kubwa katika fani ya ujenzi katika eneo la ubora na thamani ipo zaidi kwenye miradi midogo midogo kwa sababu ndio eneo ambalo miradi hii haifuati taratibu mbalimbali za kitaalamu zilizowekwa kwa sababu mbalimbali. Sababu kuu ya watu wengi ni gharama lakini sababu nyingine ya ndani zaidi ni kukosekana kwa uelewa wa hatari na madhara […]

USIOGOPE KUANZA UJENZI, ANZA NA RAMANI.

Kuna watu wengi sana hasa vijana hutamani sana kujenga lakini wanapoulizia gharama za ujenzi na kuambiwa hukata tamaa na kuamua kuahirisha kabisa kujenga. Ukweli ni kwamba gharama za ujenzi ni kubwa ukilinganisha na kipato cha watu walio wengi wa kipato cha kati. Hivyo mtu anapoangalia kipato chake kwa mwezi akilinganisha na gharama za ujenzi hukata […]

UNAWEZA KUFANYIWA RAMANI NYINGINE YA UJENZI NZURI ZAIDI YA HIYO.

Watu wengi wamekuwa wanapata changamoto kwenye kuelewa kitu kimoja katika ujenzi kwamba picha au ramani uliyoiona haikutengenezwa kwa ajili yako na hivyo sio rahisi ikufae na kwamba utaweza kupata manufaa mengi utakapofanyiwa kazi mpya inayoendana na mawazo tuliyonayo. Kuna watu pia hufikiri kwamba ramani nyumba wanayoiona inaweza kufanyiwa kazi ikibaki hivyo hivyo na ikajengwa bila […]