Entries by Ujenzi Makini

NYUMBA YA KUISHI.

Moja kati ya mambo ambayo mtu yeyote anapaswa kuyafanya kwa umakini mkubwa kwa kuzingatia ushauri bora kabisa wa kitaalamu ni pamoja na ujenzi wa nyumba ya kuishi. Hii ni kwa sababu nyumba ni kitu cha kudumu na kwa watu wengi ndio eneo ambalo utaishi maisha yako yote. Jambo hili watu wengi wamekuwa hawalipi uzito unaostahili […]

KUJENGA NYUMBA NI KAMA KUFANYA SHEREHE YA HARUSI.

Moja kati ya changamoto kubwa katika kudili na wateja wanaotaka kujenga nyumba ni pamoja na kwenye suala zima la uhitaji wa kufahamu bei halisi. Kutokana na uhalisia wa maisha yetu, wateja wengi wa kujenga nyumba huwa kitu cha kwanza ambacho huwa wanahitaji ni kufahamu bei kamili ya ujenzi wa nyumba yake ya kuishi kabla ya […]

NYUMBA YA KAWAIDA KWENDA GHOROFA.

Watu wengi hujenga nyumba zao katika wakati ambao hawana mahitaji makubwa, lakini baada ya muda watu wengi hujikuta wakihitaji nafasi zaidi kwa sababu mbalimbali. Wakati mwingine unakuta ni familia imeongezeka na wakati mwingine utakuta ni mahitaji mengine yameongezeka. Katika nyumba za kupanga wakati mwingine utakuta ni mahitaji yameongezeka sana au wateja zaidi wamelipenda eneo hilo […]

NYUMBA ZA BIASHARA NA UTAALAMU WAKE.

Moja kati ya vitu ambavyo watu wengi hawafahamu ni kwamba watu hupima hadhi zao kutokana na vile vitu ambavyo wanatumia hususan makazi yao. Watu wengi hufikiri kwamba watu hukataa kugharimia vitu vilivyo bora kwa sababu ya gharama peke yake.  Lakini ukweli ni kwamba kitu kikiwa na thamani kubwa watu wengi watajitahidi kujiongeza kulipia gharama zake […]

VIGEZO VYA NYUMBA BORA ZA KUPANGA.

Nyumba ya kupanga ni biashara na ili iweze kuwa biashara yenye mafanikio na inayolipa inapaswa kuzingatia vigezo fulani vya kiufundi sambamba na vinginevyo vitakavyowavutia wateja tarajiwa ambao ni wapangaji kwenye nyumba husika. Changamoto kubwa iliyokuwepo Tanzania na ambayo bado ipo kwa wengi ni mtazamo kwamba nyumba za kupanga ukishajenga tu itapata wateja kwa haraka ambao […]

HATUA MUHIMU KATIKA UJENZI AMBAZO NI LAZIMA KUHUSISHA UTAALAMU.

Licha ya kwamba tunahimiza sana umuhimu wa mradi mzima wa ujenzi kutumia utaalamu kuanzia mwanzo mpaka mwisho ili kuzingatia ubora na kanuni sahihi za kitaalamu katika ujenzi lakini kuna maeneo ambayo ni muhimu zaidi angalau yasimamiwe, kukaguliwa na kuhakikiwa na mtaalamu kwa sababu ndio maeneo ambayo ni rahisi kufanyika makosa, na mara makosa yanapofanyika kuja […]