Entries by Ujenzi Makini

KULAZIMISHA BEI NDOGO NI KULAZIMISHA HUDUMA MBOVU.

Wengi wetu, kutokana na mazoea na hisia zilizotutawala kila tunapofikiria kuhusu huduma za kulipia huwa tunakimbilia kufikiria ni wapi tutapata kwa bei ndogo. Lakini kwa uzoefu mkubwa tuliopitia tumeweza kuona uhalisia wake katika utekelezaji wa ile huduma husika hupelekea matokeo yasiyotarajiwa karibu mara zote. -Kwanza kabisa wale watu wenye uwezo mkubwa na maarifa sahihi ya […]

GHARAMA ITAKUWA KUBWA ZAIDI YA ILIVYOPANGWA.

Kwa kawaida katika miradi ya ujenzi huwa ni vigumu sana bajeti iliyopangwa kumaliza kazi bila nyongeza ya zaidi licha ya kujitahidi kupiga mahesabu kwa usahihi mkubwa. -Hili hutokea kwenye miradi ya aina zote kwa sababu ni mara chache sana kuweza kutabiri kila kitu kwa usahihi kuanzia muda utakaotumika, dharura zitakazotokea na mabadiliko ya bei za […]

UJENZI BORA UNAJUMUISHA VITU VINGI

Watu wengi wamekuwa hawapati matokeo wanayoyatarajia linapokuja suala la ujenzi kwa sababu wanapofikiria kuhusu ujenzi hawafikirii kwa mapana yake badala yake wanafikiria mambo machache kwa juu juu. Lakini linapokuja suala la ujenzi ili uweze kupata matoke bora na ya viwango vya juu kuna mambo mengi yanatakiwa kuhusika kama ifuatavyo; -Jambo la kwanza ni utaalamu sahihi, […]

UMUHIMU WA USIMAMIZI WA KITAALAMU KWENYE UJENZI

Kutokana na changamoto nyingi, utata kwenye swala zima la ujenzi, usimamizi wa kitalaamu katika ujenzi unachukua nafasi muhimu sana katika kuhakikisha ubora na umakini wa ujenzi husika. Usimamizi wa kitaalamu umekuwa ndio injini ya huduma za ujenzi. Baadhi ya wateja wa huduma za ujenzi wamekuwa wakitumia zaidi  njia ya kuweka fundi bila usimamizi wowote wa […]

UJENZI BORA AU BEI NDOGO?

Kwa kawaida maamuzi tunayofanya hutokana na hisia zilizojengeka ndani yetu kwa namna tulivyozoea mambo au vile tumekuwa tukiona mambo yakifanyika katika mazingira tuliyokulia. Hali hii imekuwa na changamoto sana kwani namna hii ya kufanya maamuzi kwa hisia na mazoea kumepelekea wengi kufanya maamuzi mabovu ambayo yamekuja kuwagharimu baadaye na kuwa majuto. Linapokuja suala linalohusisha pesa […]

Anza na Ramani

Unapoanza kufikiria kuhusu kujenga baada ya kuwa umepata ardhi kitu cha kwanza unatakiwa kufikiria ni ramani, na sio ramani ya kuungaunga bali unatakiwa kumtafuta mtaalamu kabisa ukae naye chini mjadili kwa marefu na kwa usahihi kuhusu kile unacholenga na namna kinaenda kutekelezwa. Hivyo kitu cha kwanza cha muhimu kabisa kuanza nacho ni ramani kwa sababu. […]

UDONGO HATARI UTAKAOLETA NYUFA KWENYE NYUMBA YAKO.

Kuna watu wamekuwa wakishangaa nyumba zao kupata nyufa ambazo wakati mwingine huwa kubwa kiasi cha kudhoofisha nyumba na kuhitaji ukarabati upya bila kujua mahali hasa zilipotokea nyufa hizo. Changamoto hii nimekutana nayo mara kadhaa ambapo wahusika wamekuwa wakipata hofu sana na wasijue hasa chanzo chake na nini cha kufanya. Kuna aina za udongo laini na […]

JE, JENGO/NYUMBA YAKO INAPANDISHA UNYEVU UNAOHARIBU RANGI YA NYUMBA?

Kuna changamoto kubwa inayozikabili nyumba nyingi hasa zilizojengwa kwenye maeneo ambayo kina cha maji hakiko mbali sana chini ardhini. Ni tatizo ambalo limekuwa sugu na hupelekea kuharibu rangi ya nyumba kwa kuanzia chini kupanda juu ambapo hupelekea nyumba kupoteza ubora wake, kushuka thamani na hata kupoteza mvuto. Sababu kubwa ya changamoto hii ni ufundi wa […]

SIFA/TABIA ZA MALIGHAFI YA VIOO.

-Uwazi, uwazi wa vioo unasaidia mtu aliyeko ndani kuona moja kwa moja nje na kifanya kuwa malighafi sahihi sana kwa paneli za madirisha, hata hivyo sifa hii inaweza kuondolewa kwenye kioo ikiwa haihitajiki. -U value(kupoteza joto), kiwango cha kioo kupoteza joto kinapokuwa juu inasaidia zaidi kwani inapunguza joto ndani ya jengo. – Uimara, japo kioo […]

MALIGHAFI VIOO

Kioo imekuwa ni malighafi inayomvutia sana binadamu tangu ilipotengenezwa kwa mara ya kwanza kwa ajili ya ujenzi miaka zaidi ya 2500 iliyopita, wakati huu ikihusishwa kuwa na uwezo wa ziada na nguvu za kimiujiza. Kioo ni kati ya malighafi za ujenzi za zamani sana wakati huo ikiwa bidhaa hadimu na ghali sana vikiwekwa kwenye nyumba […]