Entries by Ujenzi Makini

FANYA HIVI KUEPUKA KUIBIWA KWENYE UJENZI.

Watu wengi wameumizwa sana kwenye ujenzi kiasi kwamba kila wanapopanga kufanya mradi wa ujenzi wanafikiria mara mbili kwanza ni lini atapata nafasi asimamishe shughuli zake zote akasimamie mradi wake wa ujenzi ili kuepusha kuibiwa na kuharibiwa kazi. Hata hivyo bado kusimamia mwenyewe sio suluhisho kamili la kuepuka kuibiwa kwani mafundi wengi ni wazoefu sana katika […]

HIVI NDIVYO UNAVYOWEZA KUJENGA NYUMBA YA NDOTO YAKO.

Licha ya kujitahidi kutafuta sana maisha lakini watu wengi hushindwa kujenga nyumba za ndoto zao kwa sababu hushindwa kujua kwamba mradi wa kufanikisha kujenga nyumba ya ndoto yako unahitaji umakini mkubwa na kuna maeneo ya muhimu yanayopaswa kuzingatiwa lakini muhimu sana ni kupata mtu sahihi, mwenye uwezo na uzoefu wa kukuongoza kwa usahihi. Jambo hili […]

AMUA KWA USAHIHI KUHUSU MRADI WA UJENZI WA NYUMBA YAKO.

Watu wa zamani maarufu zaidi kama “wahenga” walisema majuto ni mjukuu. Na hili kila mtu anajua kwamba majuto ni mjukuu, ukweli ni kwamba mara nyingi watu huwa hawaoni uzito wa jambo au changamoto kwa kuisikia tu kwa maneno kama bado haijawatokea na ndio maana mambo yanapokwenda vizuri watu huchukulia kawaida na mara nyingi huwa hawashukuru […]

CHANGAMOTO MBILI SUGU ZA KWENYE MIRADI YA UJENZI.

Hapa nazungumzia miradi ya kawaida ambayo inaendeshwa bila mifumo imara ya uendeshaji wala kufuata taratibu za kitaaluma zilizowekwa katika utekelezaji wa mradi wa ujenzi. Ikiwa mtu atafuata taratibu zilizowekwa ambazo zinahitaji mtu yeyote anayetaka kufanya mradi wa ujenzi kuzingatia mchakato mzima kuanzia kwenye zoezi la zabuni katika kupata washauri wote elekezi wa kitaalamu kwenye ujenzi […]

KUJENGA MRADI MDOGO, KWA NINI KAMPUNI NDOGO?

Katika makala zilizopita nimeeleza sana kuhusu changamoto za ujenzi ambapo changamoto mbili kuu zimekuwa ni uaminifu na ubora. Watu wengi ambao bado hawajawahi kufanya ujenzi kwenye maisha yao wanaweza wasielewe kwa uzito unaostahili kuhusu changamoto hizi sugu sana ambazo zinaumiza sana watu kila siku. Watu ambao wameshapitia maumizi ya kuibiwa au kuharibiwa kazi au vyote […]

KWENYE UJENZI WIZI NI UTAMADUNI KWA MAFUNDI.

Kwa watu ambao ambao wameshafanya ujenzi mara kwa mara wengi jambo hili limekuwa likiwashangaza kidogo, yaani sifa kuu waliyonayo mafundi wengi kwenye ujenzi ni kufanya wizi au udanganyifu kwa kila nafasi wanayopata. Hili limekuwa likiwashangaza wengi lakini ndio uhalisia, yaani kila nafasi inayopatikana ya kufanya wizi na udanganyifu basi huwa inatumiwa vizuri bila mtu kujali […]

WIZI WA VIFAA VYA UJENZI KWENYE MRADI WA UJENZI.

Katika nchi ambayo bado maeneo mengi hakuna mifumo imara sana ya udhibiti na katika jamii ambayo imeharibika kimaadili hasa katika yale maadili ya msingi kama hizi nchi maskini za kiafrika basi moja kwa moja unategemea kwamba tabia kama wizi kwenye eneo la ujenzi itakuwa ni kubwa. Ukweli ni kwamba wizi kwenye ujenzi ni kama utamaduni […]