Entries by Ujenzi Makini

KAZI BORA YA UJENZI NI ILE ILIYOTANGULIZA UTU KABLA YA MASLAHI.

Wote tunajua kwamba binadamu wengi kwa asili tuna asili ya ubinafsi na kuangalia kile tunachokipata katika jambo lolote tunaloamua kulifanya. Hakuna tatizo kwenye tabia hii ya asili kwa sababu kwanza ndio iliyosaidia dunia kufika hapa ilipofikia. Tatizo linakuja pale ambapo asili hii inakuwa ndio kitu pekee kinachomsukuma mtu bila kujali wala kujishughulisha na ubora wa […]

MSINGI WA JENGO UANZIE JUU.

Mara nyingi watu huwa hawajui vitu vinavyopelekea jengo kuvutia au kuwa na mwonekano fulani wa kipekee unaoleta maana. Hii ni kwa sababu mvuto au uzuri wa jengo hausababishwi na kitu kimoja pakee bali ni muunganiko wa vitu vingi vilivyofanyika kitaalamu na kwa kuzingatia kanuni fulani maalum ndio hupelekea jengo kuwa na mvuto huo wa aina […]

AINA ZA UDONGO WA KURUDISHIA KWENYE MSINGI.

Baada ya msingi wa jengo kuchimbwa na kisha kumwagwa kwa zege ya chini kabisa kwenye msingi(blinding concrete) na kujengwa kwa tofali za kwenye msingi kinachofuata huwa ni kurudishia udongo kwenye msingi kujaza yale maeneo ulipoondolewa na hakujajengwa. Zoezi la kurudishia udongo kwa lugha ya kitaalamu huitwa, “backfilling”. Lakini hata hivyo mara nyingi hutokea kwamba udongo […]

KULINDWA NA SHERIA KWENYE UJENZI FANYA KAZI NA KAMPUNI KWA MKATABA EPUKA MAFUNDI.

Kisaikolojia binadamu wengi tunapenda sana urahisi, sio tu urahisi wa gharama bali hata urahisi wa michakato na urahisi wa kukamilisha jukumu husika. Kweli japo ubongo unatupeleka kwenye kutafuta urahisi kwa manufaa fulani lakini hilo mara nyingi huambatana na gharama kubwa sana. Watu wengi linapokuja suala la ujenzi mara nyingi hutafuta watu wa kawaida au mafundi […]

CHANGAMOTO ZA USIMAMIZI WA MRADI WA UJENZI.

Watu wengi kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kudhibiti na kujaribu kupunguza gharama huchagua kusimamia miradi yao ya ujenzi wenyewe. Hakuna ubaya wowote kwenye kusimamia mradi wako wa ujenzi mwenyewe na kimsingi itakusaidia sana katika kuuelewa vizuri ujenzi ambao wengi hawauelewi. Na zaidi ya hapo ni kwamba kama utakuwa makini vizuri na kutumia akili sana kusimamia […]

UNAHITAJI KUANZA MCHAKATO WA MRADI WAKO WA UJENZI SASA HIVI.

Watu wengi wana mtazamo kwamba watakuja kuanza kushughulika na miradi yao ya ujenzi wakati fulani muda ukifika. Labda wakishapata fedha au wakishanunua kiwanja/eneo wanalokwenda kujenga au labda wakishaanza mradi fulani ambao utakwenda kuwaletea pesa. Swali ni je, ni upi wakati sahihi kwako kuanza mradi wako wa ujenzi? Wakati sahihi wa kuanza mradi wako wa ujenzi […]