Entries by Ujenzi Makini

KURAHISISHA ZOEZI LA UJENZI WA NYUMBA YAKO WEKA MUDA MWINGI WA KUSHUGHULIKA NAO.

Kati ya vitu ambavyo vitakugharimu, kukupotezea muda sana na kuwa kero sana kwenye mradi wako wa ujenzi ni vikwazo utakavyokutana navyo kwa ghafla utakapokuwa unafuatilia mambo mbalimbali ambavyo hukuvitegemea na vitakavyokuwa vinahusisha usumbufu mkubwa sana ambao hukuutegemea pia na kuchelewesha sana mradi wako tofauti na ulivyokuwa unapanga na pengine hata kukuingiza hasara ya fedha na […]

KUJUA GHARAMA HALISI ZA UJENZI WA NYUMBA YAKO.

Imekuwa kawaida mtu kukupigia simu kutaka umwambie gharama ambazo mradi wake wa ujenzi utagharimu kwa ujumla kwa kukwambia mahitaji yake na hadhi ya kiwanja chake. Suala hili limekuwa lina utata kidogo kwa sababu kwanza nimekuwa nikitaka kwanza kujibiwa maswali kadhaa ambayo mara nyingi mhusika anakuwa aidha hana majibu ya moja kwa moja au hajafanya maamuzi […]

IKIWA UNATHAMINI UBORA KWENYE UJENZI, WEKEZA KWENYE USHAURI WA KITAALAMU.

Katika kufanya jambo lolote ni muhimu kufahamu sehemu ambayo inaleta matokeo muhimu zaidi ambayo unahitaji kuweka nguvu kubwa zaidi au umakini wa hali ya juu zaidi. Watu wengi wanapofikiria kuhusu ujenzi, japo kiuhalisia mwisho wa siku huwa wanahitaji sana ubora lakini huwa wakati wanafikiria kuhusu ujenzi hawafikirii sehemu sahihi ya kuweka nguvu na umakini zaidi […]

HUDUMA ZA UJENZI ZA BURE HAZINA THAMANI.

Ni kanuni ya asili kwamba vitu vinavyoweza kupatikana bure au hata kupatikana kwa urahisi sana basi thamni yake ni ndogo sana na wakati mwingine havina thamani kabisa. Hii ni kanuni ya asili ambayo sio tu kwamba nimejifunza kwenye nadharia ya vitabu bali imenitokea mara kadhaa kwenye kazi zangu za kila siku na hasa katika shughuli […]

BAJETI YA UJENZI ULIYOPANGA HAITATOSHA

Kati ya vitu ambavyo sisi binadamu tumekuwa tunapenda ni kitu kinaitwa uhakika kinachoambatana na usahihi wa vitu. Hata mawazo yetu watu wengi tukifikiria huwa tunafikiria katika uhakika na usahihi lakini kwa bahati mbaya dunia sivyo ilivyo, vitu vingi duniani huwa havina usahihi wala uhakika na ni mara chache sana kukuta kitu chochote kile chenye usahihi […]