Entries by Ujenzi Makini

VIWANJA VINGI NI VYA MAKAZI PEKEE

Kupata kibali cha ujenzi limekuwa ni suala lenye changamoto kubwa kwa miradi mingi isiyo ya makazi kwa sababu viwanja vingi ni kwa matumizi ya makazi pekee. Hata hivyo katika kununua viwanja watu wengi japo huwa na mawazo ya kuendeleza maeneo husika kwa miradi ya aina tofauti lakini huwa hawajihangaishi sana kuchunguza matumizi ya eneo hilo. […]

USIMAMIZI SAHIHI WA MRADI WA UJENZI UTAKUEPUSHA NA USUMBUFU, MATESO NA MSONGO WA MAWAZO.

Moja kati ya gharama kubwa ambazo watu huingia bila kujua ni usumbufu na msongo wa mawazo ambao hupitia pale wanapoweka usimamizi usio sahihi kwenye mradi wa ujenzi na mambo mengi kufanyika chini ya kiwango au kusababisha hasara. Usimamizi sahihi licha ya kukupatia matokeo mazuri sana mwishoni lakini pia hukuepusha kuingia kwenye msongo wa mawazo na […]

CHANGAMOTO YA UMBALI KWENYE MIRADI YA UJENZI

Kwa miradi midogo ya ujenzi mara nyingi baadhi ya watu hoona kwamba pengine wanahitaji mtaalamu anayepatikana katika eneo au mji husika, ambapo mara nyingi ni kwa sababu ya kuhofia kwamba mtu anayetoka mbali atakuwa aidha na gharama kubwa au upatikanaji wake ni wa shida. Ni kweli kwamba mtu anayepatikana karibu anaweza kupatikana kiurahisi kwa sababu […]

KAZI YA UJENZI IPANGIWE MUDA WA KUFANYIKA KWA HARAKA KADIRI INAVYOWEZEKANA

Katika mchakato wa kupitia maombi ya zabuni za wakandarasi mbalimbali wa miradi ya ujenzi kuna vigezo kadhaa ambavyo hutumika katika kuchagua mkandarasi aliyeshinda zabuni na anayestahili kupewa kazi ya kujenga mradi husika. Moja kati ya vigezo muhimu ambavyo huangaliwa ili kutoa zabuni husika ni pamoja na muda ambao mkandarasi huyo ameutaja kwamba atakuwa amemaliza kazi […]

UMUHIMU WA USIMAMIZI SAHIHI WA UJENZI HAUONEKANI, BALI MADHARA YA KUKOSEKANA KWAKE.

Changamoto kubwa iliyopo katika kuthamini ili kuweka kipaumbele kwenye huduma za usimamizi wa ujenzi ni umuhimu wake kutoonekana moja kwa moja na watu wachache sana kuweza kufikiria au kuona matokeo ya kuongezeka kwa thamani kwa sababu ya usimamizi sahihi. Kazi inapofanyika vizuri, kwa usahihi na kwa muda uliopangwa bila kuwepo changamoto yoyote kubwa ile nguvu […]

USIMAMIZI KATIKA UJENZI UNASAIDIA KAZI KUFANYIKA KWA HARAKA NA KWA VIWANGO.

Kwa sababu kazi ya usimamizi kitaalamu inatakiwa kufanyika kwa kufuata mtiririko maalum ulioandaliwa kupitia orodha ya mambo yanayofanyika ambayo ndio mwongozo wa mradi husika kiufundi na kitaalamu basi kazi haiwezi kusimama kwa sababu yoyote isipokuwa kama sababu yenyewe ni sehemu ya mradi husika. Kwa sababu kazi haiwezi kusimama kutokana na utaratibu maalumu wa kiusimamizi na […]