Entries by Ujenzi Makini

TOVUTI YETU YA UJENZI MAKINI NI KWA AJILI YA KUJIFUNZA KWA MAELEZO NA PICHA.

Katika tovuti yetu ya ujenzi makini tumekuwa tukiandika makala nyingi za aina mbalimbali kuanzia makala za kitaalamu, kiufundi, miongozo, maelekezo, ushauri n.k. Lakini pia tumekuwa tukiambatanisha na uhalisia katika picha ya vitu mbalimbali japo sio picha zote huendana na ujumbe moja kwa moja lakini angalau picha hizi huweza kujenga hamasa na kumjengea msomaji picha ya […]

HATUA TATU MUHIMU KATIKA KUFANYA KAZI YA USANIFU MAJENGO.

Katika kufanya kazi ya kitaalamu ya kufanya na kuandaa michoro ya ramani za usanifu majengo watu wengi wamekuwa wakifikiria mambo kwa ujumla zaidi ndio maana hata wengine wanashindwa kuelewa ukubwa na mchakato wa kazi nzima inavyokwenda. Katika kufanya kazi ya usanifu majengo, kazi nzima imegawanyika katika hatua tatu kubwa ambazo ni hatua ya kazi ya […]

KILA MAAMUZI UNAYOFANYA KATIKA UJENZI YANA FAIDA KUBWA MBELENI NA KINYUME CHAKE NI HASARA NA MAJUTO.

Nimekuwa nikisisitiza sana suala la kuzingatia ubora wa huduma katika kila hatua ya ujenzi. Hii ni kwa sababu nafahamu kwamba hakuna mtu aliyewahi kujutia huduma bora bila kujali alizipata kwa namna gani, kwa sababu huduma bora siku zote zitakupa furaha na ufahari baadaye. Hisia zinazotuingia na kututia hofu tukaogopa huduma bora kwa kuhofia kwa gharama […]

MIUNDO MBALIMBALI YA KISANIFU YA NYUMBA NA MAJENGO INA MAANA NA UMUHIMU FULANI KIHISTORIA.

Miundo mbalimbali inayoleta muonekano wa tofauti ikiwa ni mjumuisho wa vipengele vingi sana katika nyumba na majengo imekuwa mingi na ya aina tofauti tofauti na kila moja ikivutia watu tofauti tofauti huku mingine ikiwa na umaarufu mkubwa na mingine kuwa ya kawaida. Miundo hii imekuwa ni sehemu muhimu sana ya majengo tangu kale kabisa miaka […]

KABLA YA KUNUNUA KIWANJA PATA USHAURI KUTOKA KWA MTAALAMU WA UJENZI

Imekuwa utamaduni wa kawaida kwamba mtu anapoamua kununua kiwanja hufanya hivyo kwa kuangalia upatikanaji wa kiwanja na gharama zake bila kufikiria kile ambacho anaenda kujanga kwenye eneo husika. Ni kweli kwamba mtu huweza kununua kiwanja kwa ajili ya kujenga baadaye hivyo akili yake kufikiria zaidi kuhusu kununua kiwanja husika bila kujali kama kinatimiza vigezo vya […]