Entries by Ujenzi Makini

GHARAMA ZA MAISHA ZA JENGO.

Mara zote tumekuwa tukizungumzia gharama za ujenzi wa jengo tangu mwanzoni wakati wa kutengeneza ramani mpaka jengo kukamilika kujengwa na kuhamia, hizo ndio gharama pekee za jengo ambazo zimekuwa zikizungumzwa mtu anapofikiria kuhusu gharama za nyumba. Ni sahihi kufikiria hivyo na kweli ndilo eneo ambalo gharama kubwa kabisa ya jengo inakwenda na huwa inahitajika ipatakine […]

PUNGUZA GHARAMA ZA UJENZI KUENDANA NA BAJETI KWA KUMSHIRIKISHA MKADIRIAJI MAJENZI KATIKA KUANDAA MICHORO.

Mara kwa mara nimekuwa nikiwaambia watu mbalimbali kitu cha kwanza kinasababisha gharama za ujenzi kuwa kubwa ni ukubwa wa jengo lenyewe, yaani kadiri jengo na nafasi zake za ndani zinavyokuwa kubwa ndivyo gharama ya kulijenga inakuwa kubwa zaidi. Vitu vingine vinavyoongeza ukubwa wa gharama za ujenzi ni aina ya “design” na hasa urembo wa aina […]

KUPANGA GHARAMA ZA UJENZI.

Gharama za ujenzi ni kati ya vipengele muhimu sana kila mara mtu anapofikiria kuhusu ujenzi wa mradi wowote wa ujenzi kwa sababu, gharama za ujenzi ndizo zinazoamua endapo mradi husika utajengwa na kwa kiwango au ukubwa gani mradi huo utajengwa. Na ukweli ni kwamba gharama za ujenzi siku zote hutofautiana kati ya mradi mmoja na […]

KUJIHAKIKISHIA UNAWEZA KUWA NA MFANO WA MCHORO WA RAMANI UNAOHITAJI.

Imekuwa ni kawaida kwa baadhi ya wateja kutamani aina fulani ya “design” ya nyumba ambayo imekuwa ikiwavutia kwa muda mrefu na kuwa na ndoto ya kuijenga pale wanapoanza ujenzi lakini inapofika wakati wa kutengeneza ramani wanashindwa kuieleza kwa usahihi kwa mtaalamu husika wa kuchora na hivyo inakuwa changamoto kuifanikisha. Hakuna “design” ambayo ni ngumu kiasi […]

TAARIFA MUHIMU ZA “SIATI” ANAZOPASWA KUZIFAHAMU MTAALAMU WA UJENZI KABLA YA KUTENGENEZA RAMANI.

Ili mtaalamu wa ujenzi awe katika nafasi sahihi ya kutengeneza ramani ya ujenzi inayoendana na eneo husika la ujenzi na iliyozingatia vigezo vyote muhimu kuna taarifa kadhaa muhimu anapaswa kuzifahamu hasa kama hajafika eneo lenyewe husika. Kwanza kabisa mtaalamu wa ujenzi anapaswa kufahamu ukubwa wa kiwanja na vipimo vyake vyote vya pande zote za kiwanja […]

MADIRISHA YA ALUMINIUM NA MADIRISHA YA PVC

Madirisha ya aluminium ni aina ya madirisha yanayotengenezwa kwa kutumia malighafi ya aluminium katika fremu yake na katika ya dirisha(window panel) kunakuwa na kioo. Madirisha ya PVC ni aina ya madirisha yanayotengenezwa kwa malighafi fulani ya plastiki kwenye fremu yake wakati katikati ya dirisha husika(window panel) kuna kuwa na kioo. Aina hizi za madirisha japo […]