Entries by Ujenzi Makini

KUJIHAKIKISHIA UNAWEZA KUWA NA MFANO WA MCHORO WA RAMANI UNAOHITAJI.

Imekuwa ni kawaida kwa baadhi ya wateja kutamani aina fulani ya “design” ya nyumba ambayo imekuwa ikiwavutia kwa muda mrefu na kuwa na ndoto ya kuijenga pale wanapoanza ujenzi lakini inapofika wakati wa kutengeneza ramani wanashindwa kuieleza kwa usahihi kwa mtaalamu husika wa kuchora na hivyo inakuwa changamoto kuifanikisha. Hakuna “design” ambayo ni ngumu kiasi […]

TAARIFA MUHIMU ZA “SIATI” ANAZOPASWA KUZIFAHAMU MTAALAMU WA UJENZI KABLA YA KUTENGENEZA RAMANI.

Ili mtaalamu wa ujenzi awe katika nafasi sahihi ya kutengeneza ramani ya ujenzi inayoendana na eneo husika la ujenzi na iliyozingatia vigezo vyote muhimu kuna taarifa kadhaa muhimu anapaswa kuzifahamu hasa kama hajafika eneo lenyewe husika. Kwanza kabisa mtaalamu wa ujenzi anapaswa kufahamu ukubwa wa kiwanja na vipimo vyake vyote vya pande zote za kiwanja […]

MADIRISHA YA ALUMINIUM NA MADIRISHA YA PVC

Madirisha ya aluminium ni aina ya madirisha yanayotengenezwa kwa kutumia malighafi ya aluminium katika fremu yake na katika ya dirisha(window panel) kunakuwa na kioo. Madirisha ya PVC ni aina ya madirisha yanayotengenezwa kwa malighafi fulani ya plastiki kwenye fremu yake wakati katikati ya dirisha husika(window panel) kuna kuwa na kioo. Aina hizi za madirisha japo […]

KUPIGA JENGO PLASTA AU RIPU

Kupiga jengo ripu maarufu kama kupiga plasta ni kitendo cha kulipaka jengo zege laini ambalo ni mchanganyiko wa saruji na mchanga ili kusawazisha uso wake kwa kufukia na kusawazisha maeneo yote ambayo hayajanyooka vizuri au kukaa sawa wakati wa kujenga tofauli za kuta na nguzo. Lengo kuu la kupiga plasta ni kusawazisha uso katika “level” […]

CHANGAMOTO YA KAZI YA UJENZI IKO KWENYE USIMAMIZI.

Udhaifu mkubwa tulionao katika kufikiri namna kazi mbalimbali zinafanyika huwa tunafikiria kiufundi zaidi lakini tunasahau suala zima la usimamizi. Hii ni sawa na mtu kufikiri kuwa jukumu la mzazi kwa mtoto ni kumpa chakula, mavazi na malazi na kupuuza suala la malezi kuwa halina maana ilimradi mtoto anakula, kuvaa na kulala. Unaweza kutafakari ni kiasi […]