Entries by Ujenzi Makini

UJENZI WA NYUMBA YA KISASA, JIANDAE KUANZIA SASA HIVI USISUBIRI MUDA UFIKE.

Wote tutakubaliana kwamba mara nyingi mtu unapofanya kufanya jambo lolote huwa unakutana na vitu vingi vypya ambavyo ungetamani uvijua mapema ili ufanye maandalizi sahihi jambo ambalo lingekuweka katika nafasi nzuri zaidi kuliko namna ulivyochelewa. Kwa mfano utakuta mtu anasema ningejua hiki kiwanja kitaniletea usumbufu huu ningefanya maamuzi mapema ya kukibadilisha na kile kingine au ningeamua […]

CHANGAMOTO YA KIBALI CHA UJENZI KWENYE MATUMIZI YA KIWANJA.

Mara nyingi watu wamekuwa wakikutana na changamoto sana kwenye kupata kibali cha ujenzi pale wanapopeleka michoro ya ramani za mradi husika katika halmashauri ya jiji, manispaa au mji husika kutokana na matumizi ya kiwanja kutoshabihiana na lengo la mradi. Kuna kesi nyingine watu wamekuwa wakishangaa zaidi pale ambapo matumizi ya kiwanja yanaweza kuwa ni makazi […]

MASHARTI YA KIBALI CHA UJENZI YANATOFAUTIANA HALMASHAURI MOJA NA NYINGINE.

Halmashauri za majiji, manisapaa na miji ni taasisi zilipopewa mamlaka kisheria kwa ajili ya kusimamia mambo yote yanayotakiwa kusimamiwa na mamlaka ya kiserikali katika eneo husika. Halmashauri hizi mbalimbali nchini japo huwa na baadhi ya miongozi na mifumo inayoendana bado huwa hazifanani kwa kila kitu, kila halmashauri huwa na vikao vyake vya ndani ambavyo hupanga […]

KUPATA KIBALI CHA UJENZI KWA URAHISI PELEKA MICHORO IKAGULIWE KWANZA.

Katika zoezi la kufuatilia kibali cha ujenzi mara nyingi ni rahisi kukutana na usumbufu unachangiwa pia na urasimu uliopo katika baadhi ya halmashauri ambapo mara nyingi michoro hutolewa kasoro nyingi na kuambiwa haijatimiza vigezo vya kupewa kibali na kwamba unatakiwa kufanya marekebisho kadha wa kadha katika michoro hiyo ili iweze kupitishwa na kufikia kupewa kibali […]