Entries by Ujenzi Makini

AMUA KWA USAHIHI KUHUSU MRADI WA UJENZI WA NYUMBA YAKO.

Watu wa zamani maarufu zaidi kama “wahenga” walisema majuto ni mjukuu. Na hili kila mtu anajua kwamba majuto ni mjukuu, ukweli ni kwamba mara nyingi watu huwa hawaoni uzito wa jambo au changamoto kwa kuisikia tu kwa maneno kama bado haijawatokea na ndio maana mambo yanapokwenda vizuri watu huchukulia kawaida na mara nyingi huwa hawashukuru […]

CHANGAMOTO MBILI SUGU ZA KWENYE MIRADI YA UJENZI.

Hapa nazungumzia miradi ya kawaida ambayo inaendeshwa bila mifumo imara ya uendeshaji wala kufuata taratibu za kitaaluma zilizowekwa katika utekelezaji wa mradi wa ujenzi. Ikiwa mtu atafuata taratibu zilizowekwa ambazo zinahitaji mtu yeyote anayetaka kufanya mradi wa ujenzi kuzingatia mchakato mzima kuanzia kwenye zoezi la zabuni katika kupata washauri wote elekezi wa kitaalamu kwenye ujenzi […]

KUJENGA MRADI MDOGO, KWA NINI KAMPUNI NDOGO?

Katika makala zilizopita nimeeleza sana kuhusu changamoto za ujenzi ambapo changamoto mbili kuu zimekuwa ni uaminifu na ubora. Watu wengi ambao bado hawajawahi kufanya ujenzi kwenye maisha yao wanaweza wasielewe kwa uzito unaostahili kuhusu changamoto hizi sugu sana ambazo zinaumiza sana watu kila siku. Watu ambao wameshapitia maumizi ya kuibiwa au kuharibiwa kazi au vyote […]

KWENYE UJENZI WIZI NI UTAMADUNI KWA MAFUNDI.

Kwa watu ambao ambao wameshafanya ujenzi mara kwa mara wengi jambo hili limekuwa likiwashangaza kidogo, yaani sifa kuu waliyonayo mafundi wengi kwenye ujenzi ni kufanya wizi au udanganyifu kwa kila nafasi wanayopata. Hili limekuwa likiwashangaza wengi lakini ndio uhalisia, yaani kila nafasi inayopatikana ya kufanya wizi na udanganyifu basi huwa inatumiwa vizuri bila mtu kujali […]

WIZI WA VIFAA VYA UJENZI KWENYE MRADI WA UJENZI.

Katika nchi ambayo bado maeneo mengi hakuna mifumo imara sana ya udhibiti na katika jamii ambayo imeharibika kimaadili hasa katika yale maadili ya msingi kama hizi nchi maskini za kiafrika basi moja kwa moja unategemea kwamba tabia kama wizi kwenye eneo la ujenzi itakuwa ni kubwa. Ukweli ni kwamba wizi kwenye ujenzi ni kama utamaduni […]

KAZI BORA YA UJENZI NI ILE ILIYOTANGULIZA UTU KABLA YA MASLAHI.

Wote tunajua kwamba binadamu wengi kwa asili tuna asili ya ubinafsi na kuangalia kile tunachokipata katika jambo lolote tunaloamua kulifanya. Hakuna tatizo kwenye tabia hii ya asili kwa sababu kwanza ndio iliyosaidia dunia kufika hapa ilipofikia. Tatizo linakuja pale ambapo asili hii inakuwa ndio kitu pekee kinachomsukuma mtu bila kujali wala kujishughulisha na ubora wa […]

MSINGI WA JENGO UANZIE JUU.

Mara nyingi watu huwa hawajui vitu vinavyopelekea jengo kuvutia au kuwa na mwonekano fulani wa kipekee unaoleta maana. Hii ni kwa sababu mvuto au uzuri wa jengo hausababishwi na kitu kimoja pakee bali ni muunganiko wa vitu vingi vilivyofanyika kitaalamu na kwa kuzingatia kanuni fulani maalum ndio hupelekea jengo kuwa na mvuto huo wa aina […]