Entries by Ujenzi Makini

KIPENGELE CHOCHOTE KISICHO NA UMUHIMU KWENYE MUONEKANO WA JENGO KIONDOLEWE.

Siku chache zilizopita nilijadili kwenye makala kwamba mifumo yote inayosambaza huduma ndani ya jengo haipaswi kuonekana kwa nje na badala yake inapaswa kufichwa ndani ya mifereji wima na mifereji mlalo katikati ya nguzo au kwenye kona za jengo ambapo zitabaki kuonekana kama urembo peke yake ili kuboresha muonekano wa jengo ulio rahisi, wenye kuvutia na […]

JIHADHARI NA UTAPELI HUU KWENYE MIRADI YA UJENZI INAYOENDELEA.

Siku hizi, tofauti na miaka ya nyuma kidogo miradi ya ujenzi imekuwa ikihiatajika kupata usajili katika taasisi na bodi mbalimbali zinazojihusisha na ujenzi pamoja na mawakala wao. Mabadiliko ya sheria na taratibu yamekuwa yakitokea mara kwa mara na taasisi hizi zimezidi kufanya ufatiliaji mkali zaidi siku hadi siku kuhakikisha kila mradi wa ujenzi unafuata taratibu […]

MIFUMO YOTE INAYOSAMBAZA HUDUMA NDANI YA JENGO HAIPASWA KUONEKANA KWA NJE.

Muonekano wa jengo kwa nje, kwa ajili ya mvuto na muonekano bora haupaswi kuwa na vipengele vingine vyovyote zaidi ya vipengele vya kisanifu vilivyopangiliwa kwa ustadi mzuri kwa ajili ya kuboresha muonekano na kuleta maana inayokusudiwa ya jengo husika. Kumekuwepo na changamoto kubwa kwenye eneo hili zinaletwa na mifumo inayohusika na kusambaza huduma muhimu katika […]

FAIDA ZA UJENZI WA HARAKA(FAST TRACK CONSTRUCTION)

Ujenzi wa haraka huhusisha kazi nyingi kufanyika kwa wakati mmoja ili kuhakikisha mradi unakamilika ndani ya muda mfupi uliopangwa. Ikiwa kuna usimamizi sahihi ujenzi huenda vizuri na kwa umakini mkubwa na hivyo malengo kufikiwa na huja na manufaa yake makubwa. Faida za Ujenzi wa haraka(Fast Track Construction). Kupunguza gharama na kuongeza faida. Mradi wowote na […]

UJENZI WA HARAKA(FAST TRACK CONSTRUCTION)

Ujenzi wa haraka au “fast track construction” namna ya ufanyaji ujenzi ambapo ujenzi unaanza hata kabla ya michoro kukamilika. Lengo la ujenzi kwenda haraka ni ili kupunguza muda wa kukamilisha ujenzi husika. Njia hii ya kufanya ujenzi kwa haraka huwa inalenga kutatua changamoto ambayo inahitajika ufumbuzi wa haraka kama vile msongamano kwenye maeneo ya umma. […]

MKANDARASI ANAPASWA AWE NA WASHAURI WA KITAALAMU ILI ASIHARIBU KAZI.

Kazi yoyote ili ifanyike kwa usahihi na kwa viwango vya juu inahitaji wataalamu waliobobea katika fani husika kushiriki na kutoa ushauri wa kitaalamu katika kufanikisha kwa viwango sahihi na vinavyotarajiwa kile ambacho kinafanyika. Hili ni suala linafanya kazi katika fani zote na katika kazi za miradi yote hasa miradi mikubwa. Linapokuja suala la ujenzi mambo […]

NADHARIA YA USANIFU MAJENGO NA UJENZI.

Nadharia ya usanifu majengo na ujenzi ni ile elimu ya nadharia kuhusu majengo na ujenzi, vile namna majengo kwa ujumla yanaweza kuelezewa kwa namna mbalimbali kama vile muundo wake, aina na staili yake, utamaduni husika uliopelekea jengo hilo kuwa na muonekano, muundo, vipimo na urembo unawakilishwa na jengo husika. Nadharia ya usanifu majengo na ujenzi […]