Entries by Ujenzi Makini

KUTATUA CHANGAMOTO YA UVUJAJI WA MAJI KUPITIA “CONCRETE GUTTER” KWENYE NYUMBA AINA YA “CONTEMPORARY”.

Kuzuia maji yanayovuja kwenye paa la “contemporary house” kupitia concrete gutter, ni changamoto inayohitaji umakini, ubunifu na mbinu ya ziada kutokana na kwamba maji huwa na ung’ang’anizi na ubishi mkubwa pale yanapokutana na udhaifu wa aina yoyote ile. Baada ya maji ya mvua kushukia kwenye “gata ya zege(concrete gutter)” katika maeneo yanayopita maji mara nyingi […]

CHANGAMOTO YA NYUMBA ZA “CONTEMPORARY” MAARUFU KAMA PAA LISILOONEKANA

Miaka ya hivi karibuni kumekuwa na ongezeko la watu kupenda aina mbalimbali za “design” za nyumba huku staili ya aina ya contemporary ikipata umaarufu mkubwa kwa baadhi ya watu. Staili hii imekuwa ikipendwa sana kwa sababu ya kuvutia kwake kutokana na ule mpangilio wa “perspective lines” zinazokwenda sambamba kutokea chini mpaka kwenye paa huku paa […]

JENGO SAHIHI KWAKO NI LILE LINALOENDANA NA UTAMADUNI WAKO NA KUKIDHI MAHITAJI YAKO.

Unaweza kuwa unajiuliza sana kwamba jengo sahihi kwako ni lipi na utajuaje kwamba hilo ndio jengo sahihi na limefikia vigezo vinavyokubalika. Kwanza kabisa jengo sahihi linapaswa kuzingatia kanuni kadhaa za kitaalamu ambazo zina manufaa kwa maisha ya jengo kiufundi na kimatumizi, kisha liwe limeepuka gharama zisizo za lazima ambazo hazijaridhiwa na mteja. Jengo sahihi linatakiwa […]

KUJUA UNACHOTAKA KWENYE NYUMBA YAKO ANZA KUANGALIA UTAMADUNI WAKO WA SASA.

Imekuwa ni changamoto kwa baadhi ya watu kujua ni nini hasa wanataka linapokuja suala la nyumba yao ya kuishi kitu kinachopelekea wanakuja tena baadaye kubomoa na kuongeza baadhi ya vitu ambavyo wanafikiri wanavihitaji lakini mwanzoni hawakuvijua vizuri, ni baada ya kuanza kutumia nyumba ndio wanahisi kuna kitu muhimu kinakosekana. Pamoja na kwamba mtu huwa na […]

KUPUNGUZA GHARAMA ZA NISHATI KAMA UMEME NA NYINGINEZO KWENYE JENGO.

Kitaalamu jengo linatakiwa kutumia gharama kidogo ya nishati kadiri itakavyowezekana kutokana na ubora na usahihi wa ramani ya jengo husika ilivyofanywa na mtaalamu kwa kuzingatia suala hilo la kupunguza gharama za matumizi ya nishati, hasa nishati ya umeme ambayo ndio imekuwa inatumika kwa kiasi kikubwa zaidi kwa nyakati tulizopo. Mambo muhimu ya kuzingatia kwenye utaalamu […]