Entries by Ujenzi Makini

TUMIA NJIA YA KUCHORA NA KUJENGA(DESIGN AND BUILD) KUOKOA MUDA, GHARAMA NA KUHAKIKISHA UBORA.

Njia ya kufanya mradi kwa namna ya kuchora na kujenga(design and build), kitu muhimu zaidi cha kwanza ni kwamba itakuondolea kabisa usumbufu na kukuokolea muda ambao ungehangaika mwenyewe kuvutana na kila mtu na bado mwisho wa siku unashindwa kufikia malengo ya ubora uliyojiwekea. Sisi tutakusaidia kuhakikisha unakutana na timu sahihi imara ambayo inafanya kazi hiyo […]

FAIDA ZA KUTEKELEZA MRADI KWA NJIA YA KUCHORA NA KUJENGA/DESIGN AND BUILD

-Wataalamu wote kufanya kazi kama timu: mara nyingi kwenye miradi ya ujenzi huwa kunatokea mivutano na kutokuelewana baina ya upande wa mkandarasi(contractor) na upande wa washauri wa kitaalamu(consultants) ambayo huathiri mradi kwa namna moja au nyingine lakini kwenye njia hii ya kuchora na kujenga wataalamu wote wanafanya kazi pamoja hivyo kuepusha mivutano. -Eneo moja la […]

AINA ZA KUCHORA NA KUJENGA/DESIGN AND BUILD TYPES

Timu ya mradi inapoongozwa na mkandarasi(Contractor Led Design + Build) Katika njia ya kufanikisha mradi wa ujenzi ya kuchora na kujenga(design and build) kwa aina ya timu ya ujenzi kuongozwa na mkandarasi ambaye ataajiri na kuingia mkataba na wataalamu wengine wa ujenzi pamoja na watoa huduma wengine kwenye kufanikisha mradi huu uzito mkubwa mara huwekwa […]

KUCHORA NA KUJENGA(DESIGN AND BUILD)

Kuchora na kujenga/design and build ni njia ya kutekeleza mradi wa ujenzi ambapo mradi mzima kuanzia kuchora mpaka kukamilisha ujenzi wa mradi mzima unasimamiwa na mtu mmoja au kampuni moja inayosimama kama kiongozi wa timu nzima ya wataalamu itakayohusika kwenye mradi huo badala ya kutoa zabuni kwa kila mtaalamu anayehusika kila mmoja kufanya peke yake […]

UKARABATI WA MIFUMO YA CHUMA KWENYE JENGO(MAINTENANCE OF STEEL STRUCTURES).

Malighafi za chuma katika ujenzi huweza kuharibika kwa kupigwa kutu na kumomonyoka kiasi cha kuanza kudhoofisha uimara wa jengo ambapo kama utaendelea kuachwa utaleta hatari ya jengo kuvunjika na kuanguka. Kufanya ukarabati wa mifumo ya chuma kwenye jengo ni kazi inayohitaji umakini mkubwa na ambayo inahusisha hatua nyingi muhimu kuweza kuifanikisha. Kuna njia mbili za […]

UKARABATI WA MIFUMO YA ZEGE KWENYE JENGO(MAITENANCE OF CONCRETE STRUCTURES).

Malighafi ya zege ni malighafi inayodumu kwa miaka mingi sana hasa kwenye zama hizi ambazo teknolojia ya ujenzi imefika mbali sana, kama ikijengwa kwa kuzingatia ubora na uimara inaweza kudumu kwa karne kadhaa. Kuchelewa kufanya ukarabati wa mifumo ya zege inayoharibika hupelekea gharama za marekebisho kupanda zaidi kila siku hivyo kuwa gharama kubwa kadiri muda […]

FANYA UKAGUZI WA JENGO LAKO MARA KWA MARA.

Kufanya ukaguzi wa jengo au nyumba yako mara kwa mara ni jambo muhimu lakini wengi wamekuwa hawazingatii na hivyo wanakuja kujikuta wanalazimika kujenga ukuta kwa uzembe wa kushindwa kuziba ufa. Inapaswa kuwa na kipindi maalum cha kufanya ukaguzi wa jengo hata kama unaliona lipo katika hali nzuri kwa nje, inaweza kuwa ni kila baada ya […]

AINA ZA UKARABATI WA JENGO

UKARABATI WA JENGO -Ukarabati unahusisha kazi katika jengo ambazo zinafanyika ili kuliweka jengo katika hali sahihi inayopelekea jengo kutimiza kusudi lake au kufanya kazi kwa usahihi kwa kadiri ililivyokusiwa. AINA ZA UKARABATI WA JENGO (i)UKARABATI WA KILA MARA Hii ni aina ya ukarabati unaoweza kufanya kila inapotokea changamoto katika jengo la huduma zake, inaweza kuwa […]

UNAHITAJI UKARABATI GANI KATIKA JENGO LAKO?

Changamoto kwenye ujenzi huwa zipo mara kwa mara na mara nyingi kama kuna vitu havikufanyika kwa usahihi mwanzoni lazima huja kuleta shida baadaye hivyo kuna changamoto mbalimbali ambazo watu hupitia ambazo mara nyingi zimesababishwa na makosa yaliyofanyika wakati wa ujenzi. Tatizo ni kwamba kadiri unapoipuuza changamoto hii ndivyo kadiri inavyokuwa kuwa kubwa zaidi na kuwa […]

NYUMBA YAKO INAHITAJI UKARABATI

Kwenye fizikia kuna dhana moja inayoitwa “entropy” ambayo ni kama kanuni inayomaanisha kila kitu kilichopo duniani huwa kinaenda kikipoteza thamani yake taratibu kadiri muda unavyokwenda mbele. Sasa kutokana na nyumba kuchukua muda mrefu ukilinganisha na vitu vingine kabla ya kuanza kupoteza thamani yake basi baada ya kumaliza kujenga ni wachache ambao huendelea kufikiri kwamba watahitaji […]