Entries by Ujenzi Makini

5. UJENZI WA JENGO LINALOBEBWA NA KUTA

5. UJENZI WA JENGO LINALOBEBWA NA KUTA Hii ni aina ya ujenzi ambayo imetumika sana kwa majengo ya ghorofa miaka ya 1700 mpaka 1900 mzigo wote wa jengo unabebwa na kuta za jengo badala ya nguzo na boriti(beams). Siku hizi aina hii ya ujenzi haitumiki tena isipokuwa kwa majengo madogo ya makazi na ni kwa […]

UJENZI WA KUTUMIA MBAO NYEPESI.

Ujenzi wa kutumia mbao nyepesi ni aina ya ujenzi ambao unafanyika sana baadhi ya maeneo duniani hasa Amerika na Ulaya. Ujenzi wa kutumia mbao nyepesi una sifa zifuatazo -Ni nyepesi na unaruhusu ujenzi wa haraka, bila kuhusisha vifaa vizito. Vifaa vyote vinabebwa tu kwa mikono, ujenzi unakuwa kama kazi kubwa ya useremala. Kifaa kikuu ni […]

3. UJENZI WA KUTUMIA CHUMA NYEPESI(LIGHT GAUGE STEEL CONSTRUCTION)

Ujenzi wa kutumia chuma nyepesi ni aina ya ujenzi ambao chuma ndogo ndogo nyepesi zinapangiliwa kutengeneza pande zote za jengo. Chuma ndogondogo nyepesi zinafungwa karibu karibu kutengeneza kuta na paa la jengo husika. Kisha wanazifunganisha kwa kutumia paneli za chuma, bati au paneli nyingine. > Mara nyingi chuma hizi huandaliwa na kutengenezwa kiwandani zikiwa tayari […]

2. UJENZI WA KUTUMIA CHUMA (STEEL STRUCTURES)

-Ujenzi wa kutumia chuma hufanywa kwa kutumia chuma imara sana na yenye nguvu inayoitwa (mild steel). Chuma hizi ni imara sana kiasi kwamba ukichukua nondo yenye kipenyo(diameter) ya 1inch au 25mm unaweza kuning’iniza mzigo wenye tani 20 na inahimili. Uimara huu ni faida kubwa kwa majengo. Faida nyingine ya kutumia chuma ni urahisi wake wa […]

USIHOFIE BEI, HOFIA UBORA

Habari rafiki Linapokuja suala la sisi kufikira kuhusu ujenzi jambo la kwanza linalotujia kwenye akili zetu huwa ni bei na mara nyingi bei ndio huathiri maamuzi yetu. Leo mimi mshauri wako naomba nikushauri kitu, acha kuhofia bei, anza kwanza kuhofia ubora. –Thamani ya nyumba yako iko kwenye ubora; umekuwa ni utamaduni wetu kwa sasa moja […]

KUIMARISHA MSINGI WA JENGO(UNDERPINNING)

Hiki ni kitendo cha kuuimarisha kwa kuuongezea ubora na uimara msingi wa jengo lililopo. Kuimarisha msingi kwa kawaida hufanyika kutokana na mambo yafuatayo. -Ikiwa jengo linaonyesha dalili ya kuzama chini ardhini au kama linapata nyufa, ambapo ni dalili kwamba msingi uliopo hauna uwezo wa kubeba uzito wa jengo husika. -Ikiwa jengo linatakiwa kuongezewa ukubwa hasa […]

GHARAMA ZA UJENZI

Gharama za ujenzi, – Gharama za ujenzi hutofautiana kutokana na aina ya jengo kwa maana ya matumizi, gharama ya kujenga godown, hospitali, hotel, shule, kanisa, msikiti, majengo ya biashara, majengo ya ofisi, makazi ya watu wengi, nyumba ya kuishi na aina nyingine za majengo bei zake ni tofauti na zimeainishwa na bodi lakini nao pia […]

MSINGI WA JENGO

Msingi – Msingi wa jengo huhamisha uzito wa jengo kutoka kwenye jengo lenyewe kwenda ardhini. Msingi wa jengo huhakikisha jengo liko katika usawa sahihi na aina ya msingi wenyewe ndio huamua urefu au ukubwa wa jengo kwenda juu. Kila nguzo inayokuwepo katika jengo imejengewa msingi imara chini ambao ndio hupokea mzigo huo mzito na kuupeleka […]

UMUHIMU WA KUMILIKI NYUMBA YAKO MWENYEWE YA KUISHI

Ndugu Mdau wa Ujenzi Nyumba Bora Ya Kuishi Ni Moja Kati Ya Ndoto Ya Kila Mtu Katika Maisha. Leo Tunaangazia Umuhimu na Faida za Kumiliki Nyumba Yako Mwenyewe Ya Kuishi Kwa Wale Ambao Bado Hawajaweza Kufikia Hatua Hii Lakini Hata Wale Waliofikia ni Muhimu Kujikumbusha. -Kwanza kabisa kumiliki nyumba yako kunakupa uhuru mkubwa wa kuamua […]

AINA ZA UJENZI

UJENZI WA KUTUMIA MIHIMILI YA ZEGE Ujenzi wa kutumia mihimili ya zege ndio ujenzi maarufu na unaotumia zaidi kuliko aina nyingine za ujenzi duniani kote. Hii ni aina ya ujenzi ambapo mihimili yote ya jengo inajengwa kwa kutumia zege. Mihimili inayolala inaitwa boriti(beams) na mihimili inayosimama wima inaitwa nguzo(columns). Mihimili ambao ndio hubeba watu na […]