Entries by Ujenzi Makini

KWENYE UJENZI KUNA UJUZI/UTAALAMU NA UZOEFU.

Katika ujenzi ujuzi au utaalamu na uzoefu ni vitu viwili tofauti ambavyo vyote vina umuhimu mkubwa katika taaluma ya ujenzi kwa ujumla. Mtu mwenye ujuzi na uzoefu kwa wakati mmoja anaweza kuwa ndiye mtu sahihi zaidi na anaweza kufanya vizuri sana katika kutoa thamani ya viwango vya juu kwenye miradi ya ujenzi. Hata hivyo watu […]

AINA TOFAUTI ZA MAJENGO KWENYE GHARAMA ZINATOFAUTIANA KWENYE UKAMILISHAJI(FIISHING).

Ukifuatilia viwango vilivyowekwa na bodi mbalimbali za gharama na hasa bodi za ujenzi utakuta kwamba gharama za ujenzi kwa mita moja za mraba zimewekwa kwa makundi mbalimbali ya gharama kwamba majengo yako na gharama tofauti kulingana na malengo yake na matumizi yaliyokusudiwa. Kwa mfano utakuja ujenzi wa nyumba ya kuishi gharama yake ni tofauti na […]

MSINGI MKUU WA MAFANIKIO KWENYE UJENZI NI UAMINIFU.

Kadiri ninavyoendelea kukua kuimarika kwenye tasnia hii ya ujenzi na ukandarasi wa miradi ya ujenzi kwa ujumla ndivyo ninavyozidi kuona jinsi suala la uaminifu ni changamoto kubwa lakini likiwa ndio eneo muhimu sana la mafanikio kwenye ujenzi. Lakini pia tasnia ya ujenzi imeendelea kunionyesha jinsi suala zima la uaminifu lilivyokuwa ni bidhaa hadimu sana kwa […]

NI MUHIMU KWA MSANIFU JENGO NA MHANDISI MIHIMILI WA JENGO KUELEWANA ILI LENGO NA NDOTO YA MTEJA VITIMIE.

Watu wengi ambao wako nje ya taaluma ya ujenzi huwa hawaelewi vizuri sana namna timu ya ujenzi inavyofanya kazi na mgawanyo wa majukumu yake katika kukamilisha utaratibu na mahitaji yote ya kitaalamu kuanzia katika hatua ya michoro ya jengo mpaka wakati wa ujenzi mpaka kukamilisha. Tofauti na watu walivyozoea kwamba jengo huwa na mhandisi ambaye […]

USIENDELEE KUKAA NA MAKOSA KWENYE JENGO AMBAYO HUKUDHAMIRIA.

Japo ni kweli kwamba kufanya marekebisho yoyote ya ujenzi yanahusisha gharama ambayo mara nyingine haipo hata kwenye bajeti. Lakini ni kulihujumu na kulipunguzia jengo hadhi pale unapoamua kupuuza makosa makubwa yaliyopo kwenye jengo. Ubora na hadhi ya jengo inaongeza mpaka hamasa na shauku ya watu wanaolitumia jengo hilo kiasi kwamba inaongeza hata ile “self-esteem” na […]

SEHEMU KUBWA YA MAKOSA KWENYE UJENZI YANAREKEBISHIKA

Kutokana na kukosa uzoefu kwa pande zote mbili yaani upande wa mteja na upande wa mtaalamu anayejenga huwa inatokea kwamba baadhi ya miradi ya ujenzi inakuwa na makosa makubwa sana wakati mwingine, makosa ambayo yanaweza kuwa hayafai hata kuvumilika au yanaweza kuvumilika kimatumizi lakini yakawa ni vigumu kuvumilika kwa taswira mbaya na aina ambayo yanaleta […]

GHARAMA ZINAZOONGEZEKA KWENYE UJENZI.

Katika jambo lolote lile kwenye maisha huwa ni vigumu mtu kutabiri kila kitu kitakachotokea katika safari nzima ya kulifanya na kukamilisha jambo husika. Kuna dharura mbalimbali ambazo hazikufikiriwa kabisa mwanzoni huweza kutokea na kuathiri jambo husika kwa namna nyingi kuanzia muda, gharama na hata uelekeo wa jambo hilo. Hili limepelekea kwamba watu makini wanapokuwa wanapanga […]