Entries by Ujenzi Makini

KAZI YA UJENZI IWE NA MTAALAMU WA KUIKAGUA NA KUIDHINISHA.

Kwa miradi mikubwa ambayo inafuata taratibu zote za kitaalamu zilizowekwa na mamlaka husika hii sio changamoto kubwa kwa sababu mfumo wa kufanya kazi kitaalamu unafuatwa kwa usahihi na hivyo kudhibiti changamoto zote zinazoweza kusababishwa na udhaifu wa kimfumo. Lakini kwa miradi isiyofuata utaratibu wa kufanya kazi kitaalamu uliowekwa na mamlaka husika ambayo mingi ni miradi […]

“USIPOZIBA UFA UTAJENGA UKUTA”, VIKAO NI MUHIMU SANA KATIKA MRADI WA UJENZI.

Kuna huu msemo maarufu wa kiswahili unaosema “usipoziba ufa, utajenga ukuta” ni msemo ambao una umuhimu mkubwa kwenye baadhi ya maeneo na hapa tunaona ukiingia kwenye hili eneo la ujenzi. Katika mradi wowote wa ujenzi vikao vya kuhusu maendeleo ya mradi husika ni muhimu sana katika kuepuka kuingia kwenye changamoto kubwa au hasara kubwa. Tunafahamu […]

MAMLAKA ZA UFUATILIAJI WA UJENZI ZINATEGEMEA ZAIDI MAMLAKA ZA VIJIJI.

Mamlaka zinazohusika na kutoa vibali vya ujenzi kama vile halmashauri za miji, manispaa na majiji pamoja na bodi mbalimbali za taaluma za ujenzi kama vile boadi za uhandisi, usanifu majengo na ukandarasi ndizo zenye jukumu la kufuatilia kama mbalimbali inayojengwa imefuata taratibu zilizowekwa na mamlaka husika. Hata hivyo mamlaka hizi licha ya kujitahidi sana kufuatilia […]

NYUMBA YA GHOROFA YA KISASA, JENGA KISASA.

Kitu kimoja muhimu sana cha kuzingatia ni kwamba kujenga nyumba ya ghorofa ya kisasa ni gharama kubwa, hivyo unapofikiria kujenga nyumba ya ghorofa unafikiria kujenga kitu cha gharama kubwa kwa hiyo ni muhimu kama umeamua kuingia gharama kubwa pia ufanye kitu kizuri na cha uhakika. Kufanya kazi nzuri kunahitaji kutumia zaidi akili kuliko hisia au […]

KUONGEZEKA KWA GHARAMA KWENYE UJENZI (VARIATION)

Katika kuomba zabuni ya ujenzi(tendering) kampuni au mtu binafsi huweka gharama ambayo itamwezesha kufanya mradi husika kwa mafanikio sambamba na kupata faida baada ya kuondoa gharama zote za uendeshaji kwa kadiri ya mradi unavyohitaji. Hata hivyo kutokana na mabadiliko ya mara kwa mara yanayotokana na sababu mbalimbali kubwa ikiwa ni mabadiliko yanayojitokeza wakati mradi unaendelea […]

MAFUNDI WAZURI WA UJENZI BILA USIMAMIZI SAHIHI BADO INAWEZA KUWA NI KAZI BURE.

Kwenye baadhi ya kazi za ujenzi watu wamekuwa wakishangaa kwa nini mwanzoni waliambiwa fundi fulani ni fundi bora sana na wakati mwingine kuambiwa hata kuna kazi nzuri alifanya lakini bado mwisho wa siku ameishia kuharibu kazi aliyopewa na kuhisi waliahadaiwa na kudanganywa. Ukweli ni kwamba wakati kweli fundi huyo ni mzuri na kweli anaweza kufanya […]