Entries by Ujenzi Makini

HUDUMA BORA ZA USHAURI KITAALAMU KWENYE UJENZI ZINAHITAJI UWAJIBIKAJI WA KILA UPANDE.

Moja kati ya changamoto kubwa ambayo hasa wataalamu wa ushauri wa kitaalamu kwenye ujenzi hukutana nayo ambayo pia huchangia sana kupungua kwa ubora wa huduma hizi ni suala zima la malipo. Kutokana na kwamba kuna kazi nyingi za kitaalamu ambazo wateja hukimbia bila kulipia huduma aliyopatiwa, hili limeondoa uaminifu kwa kiasi kikubwa kwa upande wa […]

NYUMBA NDOGO ZAIDI YA FAMILIA KUJENGWA.

Kuna watu wanahitaji kujenga nyumba za familia kwa sababu tayari wana familia kubwa lakini uwezo wa kujenga nyumba ni mdogo na hivyo wanahitaji nyumba ya ukubwa utakaogharimu kiasi kidogo zaidi cha gharama. Kwa kawaida nyumba ya familia ya kiwango cha chini kabisa haipaswi kupungua chini ya angalau vyumba vitatu vya kulala, kimoja cha “master bedroom” […]

KWA NINI BAADHI YA WATU WANAPENDA KUJENGA KWA TOFALI ZA KUCHOMA?

Wapo watu wengi ambao wanapofikiria kuhusu malighafi za ujenzi kwenye suala la tofali huwa akili zinawapeleka kwenye tofali za kuchoma ambazo kwa vyovyote ndizo wanategemea kujengea nyumba zao. Unaweza kujiuliza ni kwa nini baadhi ya watu wanapenda zaidi tofali za udongo za kuchoma badala ya tofali zinatengenezwa kwa mchanga na saruji. Labda tuangalie sababu kadhaa. […]

GHARAMA YA UJENZI WA NYUMBA YA GHOROFA

Gharama ya ujenzi wa mradi ndio kitu cha kwanz aambacho kila mtu huwa anafikiria pale anapoanza kufikiria kuhusu kujenga, kitu ambacho ni sahihi kabisa kwa sababu gharama husika ndio inayoamua kama utajenga na kama utajenga ni kwa ukubwa gani au utajumuisha vitu gani. Kujua gharama ya ujenzi wa jengo lolote kanuni ya kutumia siku zote […]

UNAFUU KATIKA UJENZI WA SHULE AU TAASISI KUBWA INAYOHUSISHA MAJENGO MENGI.

Wapo watu wengi ambao wamekuwa wakifikiria kuanzisha taasisi mbalimbali na hasa taasisi za elimu hususan shule, lakini kwa bahati mbaya changamoto yao kubwa wanayokutana nayo ni kukosa uwezo wa kufadhili miradi ya kujenga shule husika. Kutokana na kukosa uwezo wa kujenga licha ya kuwa na kipaji cha kuendeleza shule husika watu wengi wamekuwa wakikata tamaa […]